NA HILI NDILO NENO LA BWANA KWAKO"Sifa mojawapo ya mtu ALIYEONGEA NA MUNGU AU KUMWONA MUNGU ni UTAKATIFU NA MABADILIKO YA TABIA.... Kila nikimtazama mtu anayesema MUNGU AMEMWAMBIA AU AMEMWONA MUNGU lakini nikikagua UTAKATIFU WAKE NA TABIA YAKE naikuta IMECHAKACHULIWA naelewa kabisa huyu ndugu HAJAKUTANA NA MUNGU bali atakuwa amekutana na "MUNGU WA DUNIA HII [SHETANI]" AU AMEDANGANYA NA HAJAKUTANA NA MUNGU KABISA…. 

Hauwezi kukaa kwenye UWEPO WA MUNGU halafu TABIA ZAKO CHAFU UKABAKI NAZO AU UKAENDELEA KUTENDA DHAMBI... Uwepo wa Mungu akijifunua ni KAMA KIOO; UTAONA DHAMBI ZAKO WAZIWAZI NA ROHO YA TOBA ITAKUINGIA NA NGUVU YA UTAKASO ITAKUGEUZA NA KUKUTOA DHAMBI HIYO AU TABIA HIYO MBOVU... Isaya alipomwona BWANA, Bila kuambiwa na mtu yeyote ALIJIONA KAMA KWENYE KIOO KUWA YEYE NI MWENYE DHAMBI NA ANA MDOMO MCHAFU, NA AKAJUA CHANZO CHA HILO TATIZO NI KUKAA KATIKATI YA WATU WENYE MIDOMO MICHAFU… 

Kwa toba hiyo MDOMO WAKE UKATAKASWA... Leo hii tunao WANAOJIITA WATUMISHI na wanasema WAMEMWONA MUNGU AU WAMEMSIKIA MUNGU [KWENYE UWEPO WAKE] Lakini BADO MIDOMO MICHAFU, TABIA MBOVU, WENYE KUPENDA FEDHA, UZINZI UNATAJWA KWAO... Hili nina uhakika HAWEZI KUWA MUNGU WETU KATIKA KRISTO YESU bali "MUNGU WA DUNIA HII" maana NAYE ANA SAUTI NA YESU ALISEMA WALIO WA KRISTO [KONDOO WAKE] HAWATAMSIKIA... UKIKUTANA NA YESU AU KUMWONA MUNGU ANAANZA KUKUBADILISHA WEWE KABLA YA KUKUTUMA KUHUBIRI, KUFUNDISHA, KUTABIRI AU KUCHUNGA KONDOO WAKE"

Mifano ya Kibiblia: Isaya 6:1,5- Isaya alipomuona Mungu alijua ya kwamba MIDOMO YAKE NI MICHAFU na alibadilishwa kuwa mtu mpya.

Luka 5:8- Petro alipomwona Yesu [Mungu katika Mwili] alijua ya kwamba YEYE NI MWENYE DHAMBI bila hata kuhubiriwa na mtu.

Matendo 9:3-22- Paulo [Sauli] Alipotokewa na Yesu kwenye maono akielekea Dameski ALIGEUZWA NA KUFANYWA MTU WA AJABU tunayemsoma kwenye BIBLIA.

Mtumishi akija akakwambia "NIMETUMWA NA MUNGU AU NIMEMSIKIA MUNGU AU NIMEMWONA MUNGU" wakati TABIA AU MAISHA YAKE HAYANA USHUHUDA WA YESU; Mwambia ndugu HUJAKUTANA NA MUNGU, NYUMA GEUKA, MBELE TEMBEA! "Ni wenye moyo safi ambao huwa WANAMUONA MUNGU" Hakuna shortcut katika hili (Waebrania 12:14, Mathayo 5:8).

Akikwambia "MUNGU ANAWEZA KUTUMIA CHOCHOTE" mjibu hivi, "MUNGU HAWEZI KUCHUKUA DIVAI MPYA [UFUNUO NA UPAKO] AKAWEKA KWENYE CHOMBO KIKUU KUU [MTU WA KALE ASIYEGEUZWA NA KUFANYWA UPYA]" Watu wa Ufunuo ni WATU WA UTAKATIFU... Full stop!

Mwl D.C.K www.yesunibwana.org dicoka@rocketmail.com +255655 466 675
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.