NI RAHISI KUFIKIRIA KUSHINDWA KULIKO KUSHINDA

 Fikiri kufaulu daima ©Shutter stock

Na Faraja Naftal Mndeme.
GK Contributor.

Watanzania na jamii yetu kwa ujumla tumejengwa na kukuzwa zaidi katika hali ya kupenda kufikiria kushindwa kuliko kushinda katika maisha yetu ya kila siku kutokana na malezi na namna mfumo wa vitu vingi wa maisha unavyoendeshwa. Mfumo wa maisha yetu tangu tunaanza nyumbani tukiwa wadogo na hata tunapoanza shule mazingira yetu hayaamini katika kushinda kuliko kushindwa.

Kujiamini katika kila tunachofanya ni kama umekuwa mzimu ulio hai unaosumbua maisha yetu tangu tungali wadogo mpaka utu uzima. Muda mwingine tumejitungia misemo ambayo ukifuatiliwa haina mashiko zaidi ya kutaka kutuondoa uoga tu na sio zaidi... "Tukiwezeshwa Tunaweza". Swali la msingi je hao waliweza waliwezeshwa na nani na wana vichwa vingapi na wamewezaje kufika hapo?


Mambo machache ambayo yanaweza kutufanya tupende kufikiria katika kushindwa zaidi kuliko katika kushinda

1. Mfumo

Mfumo wetu wa malezi kuanzia watoto na hata mfumo wa uongozi katika nchi yetu katika nyanja mbalimbali hautupi mwanya wa kuweza kufikiria na kuamini katika kushinda katika kila tunalolifanya zaidi ya kufikiria na kupenda kushindwa zaidi bila ya sisi wenyewe kujua nini tatizo limeanzia wapi.

Pamoja na mfumo mbovu katika kila nyanja ya maisha yetu ambao tumekutana nao, sio kigezo cha kutufanya iwe kisingizio kwamba tusiamini katika kushinda zaidi ya kufikiria katika kushinda... "System haipo kwa ajili ya walio nje ya system bali system ipo kuwapa favour wale waliopo kwenye ndani tu" Ni jukumu lako kuamua kubadilisha mfumo wako mwenyewe kwenye fikra zaidi kuliko kuendelea mfumo sababu utaishia kulaumu tu na hautafika kokote.


2. Maisha yetu na historia za nyuma

Familia zetu nyingi za kiafrika haziamini katika kushinda zaidi kuliko kushindwa. Ni familia bora na chache sana ambazo zinaweza kuamini katika kushinda kuliko kushindwa tangu tukiwa wadogo. Familia nyingi zimekuwa na mtazamo hafifu tangu watoto wanapoanza shule kuanzia maneno wanayotamkiwa hadi matendo wanayofanyiwa. Hii haikupi njanya ya kufikiria na uwanda mpana wa kuamini ushindi unawezeka. Utasikia wanasema, "Yaani baba yako aliishia hapo, babu hapo hapo, mimi mwenyewe mama yako pamoja na wote sisi kuwa na akili kwenye ukoo wetu bado nimeishia hapo. Je wewe utaweza au ndio unajifanya una akili sana?" Wanashindwa kujua wao ni wao na sisi ni sisi, kwani kuna vitu vingi vimebadilika sana.

Ndio utasikia hata mtu akishindwa kwenye jambo dogo tu... "Yaani sisi sijui tuna mikosi gani", hili ni tatizo kubwa katika jamii... Wewe ndio mkosi wa kwanza wa kushindwa kufanya maamuzi sahihi.


3. Makosa ya nyuma

Baada ya watu kuweza kushindwa katika maisha yetu katika kipindi fulani cha nyuma imepelekea mioyo yetu kushindwa kujiamini katika kila hatua mpya ambayo tunataka kuichukua ili kuweza kuendelea mbele. Kushindwa katika jambo fulani katika kipindi cha nyuma haina maana ya kwamba hauwezi kushinda katika jambo lingine katika maisha. Mfano, Watoto wengi wakifeli kidato cha nne huamini kuwa maisha yameishia hapo kumbe maisha bado yanaendelea.

Kumbe ni wakati wa kujaribu fursa mpya za kimaisha na mambo mengine. Imekupasa kujaribu tena katika kila unachokifanya hata kama ulishindwa nyuma, hicho sio kigezo kwamba utashindwa tena na wala sio sababu ya msingi ambayo unaweza ukaeleza watu. Fanya tena na tena.

"Mbunge wangu wa Ubungo Mhe. John Mnyika alipojaribu mwaka 2005 kugombea Ubunge kwenye jimbo la Ubungo alishindwa, lakini hiyo haikuwa tiketi ya kukata tamaa, matokeo yake mwaka 2010 alijaribu tena, ndipo ushindi ulipopatikana. Leo hii tunachekelea na kufurahia kumbe ni hatua ya mtu aliyoamua kuchukua maamuzi mwenyewe.

Jenga tabia ya kufikiria kushinda zaidi kuliko kushindwa.
God Bless Y’all
+255719742559

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.