PASTOR UCHE (DOUBLE DOUBLE) ARUDI AFRIKA YA KUSINI KWA KISHINDO

Pastor Uche akiwa na Thabo ambaye ni mtangazaji maarufu wa Radio Impact nchini Afrika ya kusini na pia ni kati ya waimbaji wa mwanzo wa kundi la Joyous Celebration.

Baada ya kuwa nje Afrika ya kusini kwa kitambo kirefu, hatimaye mwimbaji maarufu aliyelitambulisha vyema kundi la Joyous Celebration duniani pastor Uchechukwu Agu almaarufu kama pastor Uche double double, amerejea nchini humo kwa muda ili kuitangaza album yake mpya iitwayo The Glory experience.

Uche ambaye tayari alijinyakulia tuzo mbili za Crown gospel za nchini humo kupitia dvd yake iliyopita, amekuwa akizunguka kwenye vituo mbalimbali vya radio pamoja na runinga nchini Afrika ya kusini kwa mahojiano pamoja na kuizungumzia album hiyo inayoelezwa kutengenezwa kwa ubora wa hali ya juu nchini Marekani.

Kwasasa mwimbaji huyo mwenye makazi yake nchini Marekani, ameanza kuachia wimbo mmoja uliobeba album uitwao Glory ambao amekuwa akiutaja kwamba utaleta mabadiliko na watu kuutumia katika makanisa yao. Aidha katika ziara yake hiyo mwimbaji huyo alipata wasaa kutembelea makao makuu ya kundi lake la zamani la Joyous Celebration ambako alikuta waimbaji wakiwa mazoezini wakijiandaa na nyimbo mpya watakazorekodi mwezi disemba mwaka huu.

Pastor Uche akiwa kwenye mahojiano Radio CCFM asubuhi ya jana jijini Capetown.

Pastor Uche, ametamba nchini Afrika ya kusini na nje ya nchi hiyo kutokana na wimbo wake wa My God is good, wimbo ambao ulikuwa kama mlango wa huduma kufunga katika maisha yake baada ya kuanza kupata mialiko mbalimbali ndani na nje ya bara la Afrika na kuwa mmoja kati ya waimbaji wanaoongoza kwasasa barani Afrika kwa mitoko ya kihuduma.

Aidha kuna uwezekano wa mwimbaji huyo kuwepo kwenye tamasha la nyimbo za zamani za kundi hilo linalofahamika kama (MTN Joyous Rewind) ambalo hufanyika kila mwaka ingawa kwa mwaka huu bado halijatangazwa kuwepo kwake, hata hivyo kama litakuwepo kuna uwezekano mwimbaji huyo kuimba mmoja kati ya nyimbo nne ambazo amewahi kuimba na kundi hilo, huku pia mwanamama Zaza Mokhethi wa Spirit of Praise anayetamba na pambio la Calvary alionekana katika mazoezi ya Joyous kitu kinachoashiria huenda naye ameitwa kuimba wimbo wake uliompa maarufu enzi hizo akiwa na Joyous.

Pastor Uche akiwa ofisi za Joyous na moja ya tuzo za Sabc Crown ambazo kundi hilo limewahi kujishindia, pia mwimbaji huyo aliwahi kupata tuzo mbili za aina hiyo kupitia wandaaji hao.

Baadhi ya waimbaji wa Joyous Celebration wakiwa mazoezini kujiandaa na nyimbo mpya za toleo la 19 litakalorekodiwa mwezi disemba mwaka huu. Picha zote kwanisani ya Pastor Uche.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.