RAIS KIKWETE NA SHEIN WAKABIDHIWA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA SHANGWE

Marais Dkt. Jakaya Kikwete na Dkt Ali Shein mara baada ya kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa. Iwapo wananchi wataipigia kura ya ndio, basi itasomeka kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014
Historia imeandikwa kwa mara ya kwanza katika harakati za taifa la Tanzania kupata Katiba Mpya, mara baada ya marais Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Shein kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, na aliyekuwa mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel John Sitta.

Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na maelfu ya wakazi wa mji huo na vitongoji vyake, ukiachilia mbali mamilioni ya wananchi waliofuatilia kupitia runinga na vyombo vingine vya taifa limekuwa historia ya kipekee, ambapo kwa mara ya kwanza wananchi walipata kushirikishwa kwenye utunzi wa katiba ya nchi, tofauti na ile ya mwaka 1977 inayotumika kwa sasa.

Katika salamu zao, wawakilishi 15 miongoni mwa wajumbe wa Bunge Maalum waliieleza hadhira mazuri yaliyomo kwenye Katiba inayopendekezwa, wakielezea kuhusu benki ya ardhi, kutambulika kwa wafugaji, wakulima na wavuvi, uwepo wa asilimia 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume kwenye uwakilishi, uundwaji wa baraza la vijana wa Tanzania, na kadha wa kadha.

Mchakato wa kupata katiba mpya umekuwa na hatua tofauti tofauti, ambapo Bunge Maalum ndio lilikuwa na kazi ya kujadili na kuboresha Rasimu ya Katiba ambayo waliipokea kutoka kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Licha ya mvituano mikali ambayo ilidhaniwa Bunge litavunjika na mchakato kushindwa kuendelea, bado hatima ilifika ambapo kura zilipigwa na kufikia hatua ya kupitishwa rasmi, hivyo kuwa na nyaraka ambayo itawafikia wananchi kwa ajili ya kuamua kama wamependezwa nayo ama la.

GK ilikuwepo, na itakuletea picha na habari kamili. Endelea kuwa nasi.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.