ROSE MUHANDO SASA AJA NA JIWE

Muimbaji maarufu namba moja wa Afrika Mashariki wa nyimbo za injili amefyatua kibao cha pili kingine kilichotengenezwa katika studio za Sony Music Africa, ambapo kibao cha kwanza kiliitwa Wololo kilichobeba albam ya Yesu Kung’uta, chini ya usimamizi wa Rock star 4000.

Wimbo wa jiwe umetengenezwa na kuchezwa na Rose Muhando ambapo kupangiliwa na kuzalishwa na Yusuph Mayige katika Studio ya Sony Music Afrika na kuendelezwa na kuongezewa vionjo na Rockstar 4000.

"Rose Muhando asema wimbo huu unatambulisha kuwa naniataendelea kuitawala hii dunia na kila kilichomo ndaniyake, katika dunia hii ya sasa , tunapoteza uaminifu nakumsahau Mungu katika kutawala kila kitu. Ni miminatakiwa kuweka muda wa kumkumbuka na kumsifuyeye kwa njia ileile tunayotumia katika kusifu nyota zetukwa majina tunayoyajua wenyewe ila mungu wetu nimkuu kuliko majina yote makuu, Mungu Mwamba, “Jiwe”.

Rose Muhando amejulikana kuwa msanii mahiri na wa kwanza Afrika Mashariki na pia amefanikiwa kukutana na viongozi wakubwa wa serikali akiwemo Mheshimiwa Rais wa muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete, Rais mstafu wa Kenya mheshimiwa Daniel Arap Moi na viongozi wengi wa siasa.

Kwa takwimu ya usambazaji wa muziki Rose Mhando amekuwa msanii wa kwanza kuongoza mauzo ya muziki wa injili Afrika mashariki.

DVD ya albamu yake inatarajiwa kufyatulia msimu wa krismasi. 
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.