SABABU 5 KWANINI WATU WENGI NI MASIKINI (1)

SABABU 5 KWANINI WATU WENGI NI MASIKINI

1. Wengi wanaishi maisha YA KUCHEZEA NA KUTOTHAMINI VICHACHE MUNGU ALIVYOPITISHA MAISHANI MWAO.
Mwalimu Dickson Kabigumila
"Yesu alipofanya muujiza wa kulisha wanaume 5000; Chakula kilichobaki alikikusanya na ALISISITIZA KISIPOTEE HATA KIPANDE KIMOJA CHA MKATE" (Yohana 6:8-12). -Mtu yeyote ASIYETHAMINI VIDOGO MUNGU ALIVYOPITISHA MIKONONI MWAKE NA KUVIHIFADHI KWA UMAKINI NA ADABU hawezi kamwe kuwa tajiri; Atakuwa masikini milele! Je, Wewe unavitunza vitu vidogo ambavyo Mungu anavipitisha mikononi mwako au unatupa ovyo? Hauwezi kuwa na hekima ya uchumi na maisha kuliko Yesu; YEYE HAKURUHUSU HATA KIPANDE KIPOTEE! Badili hiyo tabia yako ya UFUJAJI NA UHARIBIFU KAMA UNATAKA KUTOKA KWENYE UMASIKINI. "Ni matone madogo madogo ya maji yanayotengeneza bahari kubwa ya maji unayoiona"
2. Wengi wanaishi BILA MIPANGO, WANAISHI MAISHA YA BORA LIENDE. Je, Umewahi kumwona mjenzi yeyote aliyejenga nyumba bila ramani? Je, umewahi kumuona mjenzi yeyote aliyejenga bila kupima? Kwanini iweko RAMANI? Kwanini viweko VIPIMO MAALUMU? Jibu ni rahisi, UKITAKA KUJENGA MAISHA YAKO YA UCHUMI NA FEDHA, HAUNA TOFAUTI NA MJENZI WA NYUMBA.
Hii ndiyo sababu ukitaka mkopo benki au taasisi nyingine ya fedha watakuuliza kuhusu WAZO LA BIASHARA [business proposal and idea] ambayo wataalamu hao wa fedha wataitumia kupima UWEZO WAKO NA MIPANGILIO YAKO YA KIFEDHA inayokustahilisha kupata fedha au la! Yesu alisema, "MTU AKITAKA KUJENGA NYUMBA, HALAFU ASIHESABU KWANZA GHARAMA SAWASAWA, AKIKWAMA KUIMALIZA WATU WATAMCHEKA NA KUMDHIHAKI NA ATAPATA AIBU YA MWAKA" (Luka 14:28).
Mungu wetu ni Mungu wa Mipango; Ilipoingia dhambi kule bustanini, hapohapo alitangaza MPANGO WA WOKOVU KUPITIA UZAO W MWANAMKE. Usipokuwa na mipango yoyote ya maana na ya kueleweka maishani, tayari umekwama na haikosi utakuwa na umasikini wa kukutosha! "UKISHINDWA KUPANGA, UMEPANGA KUSHINDWA" "Haijalishi unapata hela kiasi gani au pesa kiasi gani inapita mikononi mwako; Kama haujaipangilia na kuielekeza pa kwenda, itapotea hivyohivyo" WEKA MIPANGO YA MAISHA YAKO; HAKUNA WA KUKUPANGIA.
3.Kujaribu KUISHI MAISHA YALIYOKUZIDI. Watu wengi wanaishi maisha ya kutaka kujionesha, kutaka kuwakoga watu au kutaka kuonesha wengine kwamba NAO WAMO. Tajiri ni yule mtu ambaye amefanikiwa KUISHI AWEZAVYO NA SI WATU WATAKAVYO. Tajiri ni yule anayeishi kwenye ndoto zake na maono yake bila kujali watu wanamuelewa au hawamuelewi. Tajiri ni mtu anayeishi maisha yake halisi kwa wakati uliopo. Biblia inasema, "UTAUWA NA KURIDHIKA NI DAWA BORA...." (1Timotheo 6:6). Mtu atakayekuwa na MOYO WA KURIDHIKA NA KUTOJARIBU Kuishi maisha yasiyokuwa yake, Maisha yaliyomzidi; Mtu asiyeishi maisha ya kujikweza, huyu ndiye atakayekuwa na MAISHA MAZURI YA UCHUMI. "Ridhika na hali yako uliyonayo sasa na usijaribu kukopa au kuomba ili uishi maisha ya juu"
4. Kutokupenda KUFANYA KAZI NA UVIVU. Unajua kuna watu wanatoa sana ZAKA NA DHABIHU lakini hawapati matokeo kwenye maisha yao; HAWANA "CHANEL/ MKONDO" ambao Mungu atautumia KUWAPATIA BARAKA ZAO. Hawana GHALA ambayo MUNGU ATAIMIMINIA BARAKA MPAKA KUSIWEKO NAFASI (Malaki 3:10). Hawana KAPU LA UNGA ambalo MUNGU ATALIBARIKI ILI LISIISHIWE (Kumbukumbu 28). Hawana MZABIBU ambao MUNGU ATAULINDA USIPUKUTISHE KABLA YA WAKATI WAKE (Malaki 3:11), Hawana HAZINA [VITEGA UCHUMI] amabazo MUNGU ATAZIJAZA (Mithali 3:9-10). Kanuni ya Biblia inasema, "USIPOFANYA KAZI NA USILE" (2Thesalonike 3:10-11). Hata mimi mtumishi wa Mungu nafanya kazi yangu kwa bidii na Mungu ananitunza na kukutana na maisha yangu hukuhuku madhabahuni, USIPOKUWA NA SHUGHULI YA KUFANYA, UNAMBANA MUNGU ASIPATE MKONDO WA KUPITISHIA BARAKA ZAKO baada ya kutoa ZAKA NA DHABIHU ZAKO... Mungu anataka kubariki CHANZO CHA MAPATO YAKO; Hivyo usipofanya kazi, Usipojishughulisha, UNAZUIA upako wa wa Mungu kukupa utajiri! "FANYA KAZI NA FUNGUA VYANZO VYA UCHUMI AMBAVYO MUNGU ATAVITUMIA KUPITISHIA BARAKA ZAKO; UWE NA HAZINA ATAKAYOIJAZA BWANA; UWE NA KAPU LA UNGA ATAKALOLIBARIKI MUNGU" Kufanya kazi ni lazima, Iwe ya kujiajiria au kuajiriwa!
5. MTAZAMO NA IMANI POTOFU KUHUSU UTAJIRI, MALI NA PESA. Makanisa mengi yanapinga habari ya utajiri na pesa. Wengi utawasikia wakisema, "Hizi injili za utajiri si nzuri zinapotosha watu" Lakini Yesu alisema, "NIMEKUJA ILI WAWE NA MAISHA KISHA WAWE NAYO KWA KIWANGO CHA JUU SANA" (Yohana 10:10 Biblia za Kiingereza). Yesu alipoanza kuhubiri Injili alisema, "NIMEKUJA KUWAHUBIRIA MASIKINI HABARI NJEMA" (Luka 4:18-19), HABARI NJEMA KWA MASIKINI NI KUMTOA KWENYE HALI YAKE MBAYA ALIYONAYO KIROHO KWANZA HALAFU KIUCHUMI. Hii ndiyo Injili halisi aliyoileta Yesu, Haikatazi watu kuwa na UCHUMI MZURI NA MKUBWA. Ukisoma Kitabu cha Yakobo, Biblia inatwambia, "NDUGU YAKO AKIWA UCHI UMVIKE NA USISEME ENENDA KWA AMANI UKAOTE MOTO NA MUNGU ATAKUSAIDIA" Lakini hii ndiyo INJILI tunayohubiri makanisani. HATUNA MAJIBU YA KIUCHUMI NA MAHITAJI YA WATU WASIOJIWEZA; HII SI SAHIHI. Yesu na wanafunzi wake WALIKUWA NA HUDUMA YA KUWASAIDIA WASIOJIWEZA. Mitume wa Yesu WALIKUWA NA HUDUMA YA KUWASAIDIA NA KUWATUNZA WASIOJIWEZA. Hii ni huduma yetu kama KANISA LA SIKU ZA MWISHO, Lazima tuwe na majibu ya KIROHO NA UCHUMI ya dunia yetu kama Yesu na Mitume. Hivyo kuwa na pesa, utajiri na uchumi mzuri NI LAZIMA ili kurahisisha kazi ya INJILI tuliyokabidhiwa katika siku za mwisho. YESU MWENYE ALIKUBALI KUFANYIKA MASIKINI NA AKAISHI MAISHA YA CHINI KWA AJILI YETU, ILI KWA UAMSIKINI WAKE SISI TUPATE KUWA MATAJIRI (2Korintho 8:9). INJILI KUIPELEKA NA KUWAPELEKA WATENDA KAZI VYOTE VINAHITAJI PESA, NI GHARAMA (Warumi 10:13-17). Asikudanganye wala kukupumbaza mtu, kuwa tajiri na kuwa na uchumi mzuri ni bora mara elfu kuliko kuwa masikini na kuomba omba! Kuwa na vingi kwa utele kiasi cha kugusa na kubariki wengi kwa yale aliyokujalia Mungu ni baraka sana kuliko kuwa katika nafasi ya kupokea misaada. Fedha si mbaya, Bali kuifanya pesa kuwa muungu kwako na ikachukua thamani ya Mungu na muda wa Mungu, hilo ndilo tatizo kubwa! MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE, KWA AKILI YAKO YOTE, KWA NGUVU ZAKO ZOTE NA KWA MALI YAKO YOTE. Ukiweza kutimiza hili, PESA HAITAKUPA SHIDA maana utajua kwamba WEWE NI WAKILI TU WA MALI YA BWANA!
Kwa leo niishie hapa, Tafakari na ujifunze, Mwl Dickson Kabigumila. +255 655 466 675 (Kupiga, Whatsapp, text na viber). dicoka@rocketmail.com (email) Website: www.yesunibwana.org
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.