SAFARI YA DENNO NA EUNICE NJERI NDIO CHAGUO LA GK

Dennis "Denno" Karanja
Habari ya Jumapili mpenzi msomaji, tunatumai upande wako kuna uzima. Na kama ndivyo basi sifa na utukufu zimrudie Mungu. Kama sivyo basi tambua kwamba kuna sababu kwa kila jambo, na katika hilo ndipo Chaguo la GK linakujia, Safari kutoka kwake Dennis Karanja 'Denno' akimshirikisha mwanamama Eunice Njeri.

Kwa ufupi wanaeleza kwamba, "Shida nyingi safarini, ingawa safari ngumu nitafika" na ndivyo ilivyo na kwako badi. Shida nyingi safarini, ingawa safari ngumu, kufika lazima ufike, maana hata Biblia inaeleza kuwa mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.Muimbaji Denno ni mlemavu wa macho, laini hili halijamzuia kumsifu Mungu, wewe una ratiba gani na Mungu kwa kipawa alichokupa? Tunakutakia Jumapili yenye majibu na baraka kwa maisha yako na wanaokuzunguka.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.