SHANGWE ZA GK MIAKA 12 YA MWANAMAMA WA WIMBO CALVARY

Hivi karibuni mwanamama aliyeimba pambio maarufu za Calvary kutoka nchini Afrika ya kusini aitwaye Zanele Mokhethi  Masike ama maarufu kama Zaza alitimiza miaka 12 ya ndoa yake na mumewe bwana Masike, ndoa ambayo walihitimisha kwa kuhudhuria kanisani kisha kuwa na mda na marafiki zao kusherehekea na kuwapongeza maharusi hao kwa miaka 12 ya ndoa yao.

Wakati huo huo mwanamama huyu wiki hii alipendekezwa kuwania tuzo kupitia tuzo maarufu za injili nchini Afrika ya kusini ziitwazo Crown gospel awards akipendekezwa kwenye vipengele vya mwimbaji bora wa muziki wa injili pamoja na mwimbaji bora wa kike. Safari ya Zaza kimuziki imeinuliwa zaidi kupitia kundi analoimbia kwasasa la Spirit of Praise ambalo tayari limeachia DVD mpya huku uzinduzi kamili wa DVD hiyo ni tarehe 1 November katika ukumbi wa Rhema Auditorium.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.