SHANGWE ZA GK NI EMMANUEL NA STAR MUNISY SHEMDOE 'WATUMISHI'

Shangwe nyingine jumamosi ya leo ni zao bwana Emmanuel Shemdoe na mkewe mpenzi Star Munisy wakitimiza miaka minne ya ndoa yao waliyofunga tarehe 10 october mwaka 2010 wote wakiwa waimbaji wa kwaya ya Vijana Kijitonyama lutherani jijini Dar es salaam usharika ambao pia ndipo walipofungia ndoa yao. Maharusi hawa Mungu amewabariki watoto wawili mpaka sasa.

Star Munisy ni mwimbishaji katika kwaya yake ya vijana Kijitonyama, lakini pia amefanikiwa kurekodi album yake binafsi nje ya kundi, hakika ni album nzuri sana kutokana na mwimbaji huyu kubarikiwa sauti nzuri sana ambayo inaweza kumsimamisha mtu yeyote atakayemsikia akiimba. Habari zaidi juu ya kanda yake utazipata hivi karibuni. GK inawatakia maisha marefu maharusi hawa.

Familia yenye furaha, bwana na bibi Shemdoe na binti yao wa kwanza daktari Daniella.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.