SHANGWE ZA GK: SABABU 10 ZA KUOA AMA KUOLEWA

© Truth Dispach
Mitaa mbalimbali imeshasikika watu wakisema kwamba hawatokaa waoe ama kuolewa. Hii inatokana na sababu mbalimbali ambazo zimewapelekea kusema hayo, ikiwemo athari za kisaikolojia kutokana na mifano isiyo mizuri waliyoshuhudia kwa wanandoa. Katika pitapita mitandaoni, GK inakuletea sababu kumi kwanini uoe ama kuolewa kwa mujibu wa Women's Life.

1. Maisha marefu zaidi
Inakadiriwa kwamba idadi ya watu wanaofariki ni kubwa kuliko ya waliopo kwenye ndoa. Wanandoa wanapendana na hivyo kujaliana na kusaidiana kila mara msaada unapohitajika. Watu wanaohisi kuwajibika kwa ajili ya wenza wao na watoto wao pia hujiweka kama mazingira salama, maana wanajua kuwa wanahitajika sehemu. Ushauri: Ukitaka kuishi maisha marefu zaidi, oa ama olewa. Ila la muhimu usije ukaoa au kuolewa na ambaye hauna mapenzi ya kweli kwake.

2. Kujipenda
Takwimu zinaonesha kwamba wanandoa wana afya. Baadhi ya wanandoa huhisi kuwajibika kwa wenzao kiasi kwamba wanaanza kujipenda pia wenyewe kwa kuachana na tabia mbaya, jambo ambalo linapelekea kuishi maisha marefu zaidi. Ni hatari kuwa kwenye mahusiano ambayo watu hawaelewani na pia wanatendana; hapa maisha yatakuwa mafupi na yasiyo na afya kabisa. Hoja hapa si kuoa ama kuolewa ili mradi tu, ila kwa ajili ya kufurahia maisha ya ndoa, kumpenda mwenza wako na kupendwa pia.

3. Kuepukana na magonjwa ya zinaa
Wanandoa hukutana kwa tendo la ndoa mara kwa mara, na hivyo hawahitaji kutafuta hitaji la namna hiyo nje. Hili linapunguza uwezekano wa maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Hapa tunazungumzia wanandoa ambao wanapendana na pia ni waaminifu kwenye ndoa yao. Wanaochepuka mara zote wanakuwa kwenye hatari ya kueneza maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

4. Afya bora kwa wananake
Kwa wanawake, kuna faida ya kiafya nyingi za kuolewa. Maisha mazuri ya ndoa yanathibitisha kuleta utimilifu wa furaha ya ndoa. Hii pia inasaidia kuinua "mood". Si kwamba afya ya akili haina umuhimu zaidi ya afya ya mwili. Utafiti umethibitsha kwamba watu ambao hawajaoa ama kuolewa wanapatwa na matatizo ya mfadhaiko zaidi. 

5. Afya bora kwa wanaume
Si tu kwamba wanawake ndio wanafaidi kuwa ndani ya ndoa, ila pia ni afya kwa wanaume kiakili na kihisia pia. Wanakuwa na mtu wa kuwajali na hata kupendwa pale wanapohitaji. Hii ni nzuri kwa mzunguko wa damu wa mwanaume, jambo ambalo linapelekea kupungua kwa baadhi ya magojwa ambayo angeweza kuumwa, ikiwemo shinikizo la damu.

6. Uchumi ulio bora
Ni jambo lililo wazi kwamba wawili wanatumia pesa zaidi ya mmoja. Lakini ni dhahiri kwamba wanandoa wanapata pesa zaidi na kuweza kujikimu na kununua zaidi. Wanaume waliooa na kuwa na watoto wanatambua ya kwamba wanahitaji kuhudumia familia kwa mahitaji yote, na hivyo wanachakarika zaidi kwenye kazi ili wapate kiwango cha ziada, tofauti na ilivyo kwa mwanaume ambaye hajaoa - ambaye huenda ameridhika na anachokipata kwa kuwa yuko peke yake.

7. Kuzishinda tabia mbovu
Baadhi ya tafiti zinaonyeshwa kwamba watu huachana na tabia zao zilizo mbaya kwa urahisi zaidi kutokana familia zao kutowaruhusu kufanya hivyo, mathalani kuachana na pombe na sigara. HIli linatokana na aidha watoto ama mke au mume kumshauri na kumhamasisha afanye hivyo. Kama mtu huyu angelikuwa peke yake bado, ingelikuwa ni ngumu zaidi kupambana na tabia ambazo zinamsumbua. Ni vita ngumu.

8. Urahisi wa kulelea watoto
Unapokuwa na mwenza, ni rahisi zaidi, hasahasa tukizungumzia watoto wanaokuwa. Wazazi wanaolela watoto wao kwa oamoja hufanikiwa kwa kiwango kikubwa na kuwa mfano bora kwa watoto wao. Watoto hujifunza maana halisi ya familia, jambo ambalo huwafanya wenye furaha na kukuza familia zao vema wawapo watu wazima.

9. Maisha yalijitosheleza
Kwa kuwa kwa pamoja wanandoa wanapata pesa zaidi au ilivyokuwa awali wakiwa peke yao, basi ni rahisi kutimiza mahitaji yao - ikiwemo kuwa na nyumba yenye kukidhi mahitaji yao, chakula kizuri, na hata elimu bora kwa ajili ya watoto wao.

10. Mwenza wa milele
Ni jambo jema kuwa kwenye mahusiano na mwenza wako, tena ambaye yupo muda wote kwa ajili yako akikulinda na kuwa sababu ya wewe kuamka na jukumu. Hii ni zawadi ya milele. Hakuna furaha kama kuwa na mtu ambaye umeamua kudumu naye kwenye maisha yako yote, huyo ni wa kipekee sana.

Sababu hizi kumi zimenakiliwa kutoka Women's Life, huenda ukawa na sababu za ziada kuhusu kuoa ama kuolewa. Tushirikishane kwenye maoni hapo chini.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.