SHETANI KURUDISHA ALICHOKUIBIA, NI WEWE KUPIGANIA MATEKA WAKO


Ukiona Mtu ni mgonjwa ujuwe ni Mtu aliye ibiwa afya yake,ukiona Mtu ni masikini ujuwe ni Mtu aliye ibiwa mafanikio yake,ukiona Mtu anamateso ujuwe ni Mtu aliye ibiwa uhuru wake,
Isaya 42:22 inasema...

Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa;wote wamenaswa katika mashimo,wamefichwa katika magereza,wamekuwa mawindo,Wala hapana aokoaye,wamekuwa mateka Wala hapana asemaye,rudisha.

Mpaka umepigana vita vinginevyo uwezi kumiliki na kulinda ulichonacho,labda umeibiwa afya yako na shetani akakupa ugonjwa,au biashara au kazi au ndoa au watoto au elimu au Mali zako,ndugu kutawala au kumiliki na kurudisha ulichoibiwa ni kupigana kurudisha,
Ibrahimu ndugu yake alitekwa alichofanya ibrahimu ni kwenda kupigana ili arudishe,

Mwanzo 14:15-16 inasema...
Akajipanga apigane nao usiku,yeye na watumwa wake,akawapiga,akawafukuza mpaka hoba,ulioko upande wakushoto Wa Dameski,
Naye akarudisha Mali zote,akamrudisha na Lutu nduguye na Mali zake,na wanawake pia na watu,
Kama ndugu unataka kurudisha afya yako ni mpaka umepanga vita ufanye vita na adui aliye kuibia,umasikini matatizo yataondoka kwa kupigana kuikataa hiyo hali.

Ayubu 20:15 inasema .....
Amemeza Mali,naye stay atapokea tena,
Inawezekanaje atapike Kama ujampiga na kumtapisha?
Kile ambacho una ni kile shetani amemeza ndugu si wakati Wa kulalamika kusema eti magonjwa yapo kwa sababu ya hali ya hewa au dunia imebadilika au ni vyakula tunavyokula,wewe usidanganyike umeibiwa,siyo kwa sababu ulizaliwa kwenye familia masikini we acha hiyo baba yako hakujuwa kudai walichoibiwa,ni wakati wako kupigana na walioibia ukoo wenu,
Biblia inasema hivi…

Isaya 14:17
Aliye ufanya ulimwengu ukiwa,akapindua miji yake;
Asiyewafungua wafungwa wake waende Kwao?
Ndugu nimejaribu kukuonyesha ili uelewe kuwa chochote unachetesekea Leo ni kile alichochukua shetani umeona hapo hawana chi wafungwa zake waende kwa hiyo kutoka kwenye ufungwa uwe Wa magonjwa au umasikini au utasa na mengineyo hiko haki yako ni Yesu alipokuja msalabani akafa ili wewe uwekwe huru na kila kitu chako,Yoh 10:10 Mimi nalikuja ili muwe na Uzima kisha muwe nao tele,Yesu anasema,

Katika Jina la Yesu pokea Nguvu ya kukuwezesha kupigana vita na ushinde katika Jina la Yesu ameni.
Tutaendelea na ili somo mpaka kimeeleweka kwako katika Jina la Yesu.
Ubarikiwe.


Ujumbe kutoka kea King Sam.

Kama unataka niwasiliane na wewe kwenye simu namba yangu hii hapa +447903180067
Namba ya whatsapp hii +447977225185
Ubarikiwe na Yesu

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.