SOMO: SHERIA MBILI ZA ROHONI - MCHUNGAJI GWAJIMA

Mchungaji Josephat Gwajima
Kuna ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili. Mtu anapofanikiwa rohoni baadae anafanikiwa mwilini. Inaweza kuwa magonjwa au ukawa na matatizo yakikutokea mwilini jua kuwa yameanzia rohoni. Unapoanza kuomba na kushambulia lazima utambue kuwa unashindana na ulimwengu wa roho.Imeandikwa;

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Waefeso 6:12
Kumbe kabla ya kubarikiwa lazima ubarikiwe rohoni. Tukizungumzia miji ya kiroho, inamaana kwamba ulimwengu wa roho ni sawa na miji unayoiona hapa duniani. Ukiona watu wanajua maneno au mistari ya biblia yote, sio ishara ya kuwa yeye anauwezo wa kuyajua yote na namna ya kushindana. Mungu ni roho, hivyo lazima tumwabudu katika roho. Imeandikwa.
Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; Yohane2:24
Viumbe katika ulimwengu wa roho mfano, Mungu, malaika, mashetani
Viumbe wa kimwili ni kama wanadamu, kuku, simba, miti

Katika ulimwengu wa roho, kuna sheria mbili zinazouongoza. Mambo yote huanzia katika ulimwengu wa roho, hasa katika ndoto. Zipo sheria 2, zinazoongoza ulimwengu wa roho.

1. KUBADILIKA UMBO NA KUVAA UMBO LOLOTE
Ili mashetani ambao ni wachawi ili waweze kwenda kuroga lazima watoke ndani ya miili yao na kuvaa umbo jingine. Kwa kuwa anakuwa rohoni anaweza kuvaa umbo lolote, na kugeuka kuwa kitu chochote. Mfano, paka, mbwa, kunguru. Lakini wachawi wanaposikia hukutambua kuwa ni wachawi wanafurahi sana. Imeandikwa; Marko 16:12

12 Baada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba.

Yesu aliwatokea wanafunzi wake akiwa na sura nyingine, lakini kwa kuwa alikuwa rohoni, alionekana kuwa na sura nyingine. Yesu anasura nyingine, kama umezoea kumuona daktari leo anasura nyingine, akitaka kukutokea kama mmea natakutokea kama ua la sharoni, au mzee wa siku, lazima utambue kuwa laizima atokee kwa sura nyingine.

Ukiri; leo katika jina la yesu yesu akutokee kwa sura nyingine, kama umezoa yesu ni mponyaji tu leo anasura nyingine, ni mfariji, ni mfalme wa wafalme, ni mwamba wa kale. Leo lazima yesu atokee kwa sura nyingine sawa na tatizo ulilonalo. Amen.

Yesu aliamua kubadili sura lakini wanafunzi wake walijua ni yeye. Kila unapoongezeka kila hatua unaongeza marafi unaongeza maadui pia. Lakini kama ulikuwa umezoea kutembea kama chura tambua kuwa unatakiwa kuruka juu kama tai. Imeandikwa;……………………………. Yohana20;15
15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.

Nirahisi sana watu kukuamini lakini mtu aliyekuzoea hawezi kukuamini kirahisi, ndiyo maana Yesu alimtokea mama yake kwa sura nyingine kama mtunza bustani, ili aweze kumwamini. Watu wamemzoea yesu wa kuponya magonjwa tu lakini yesu anatokea kwa sura nyingine ili mambo yaweze kutokea na kumwamini.

Hivyo ili uweze kufanya ya rohoni lazima uvae sura nyingine. Imeandikwa; ufunuo 1:9
9 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
Roho inaweza kuvaa sura yoyote ndiyo maana Yesu alimtokea Yohane katika sura nyingine kwenye kisiwa cha Patmo.. Imeandikwa;

Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, Mwanzo18; 1-2
Kumbe roho inaweza kugeuka na kuwa kitu chochote, na kufanaya kazi kama wanadamu. Imeandikwa; 

Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali. zaburi 104:4
Ukishaona matukio kama hayo unahisi ni upepo kumbe kuna watu ndani ya upepo. Unaweza kuona upepo unakuja ukahisi ni upepo kumbe ni mjomba au bibi yuko ndani ya upepo. Lazima utambue kuwa kuna upepo unaosumbua hali ya maisha yako ndo maana unaona taabu na misukosuko.
Yesu alisema na tuvuke ng’ambo ya pili lakini shetani aliyajua hayo na kutikisa chombo. Tambua hata wewe kwenye maisha yako ukiona umepanga kufanya jambo lolote la maendeleo na mara gafla matatizo yanaanza usikubali pigana maana ni upepo huo umetengenezwa ili usifike unakoenda au usifanye unachotaka kufanya. Imeandikwa;

Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao. 

12 Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao. Kutoka 7; 11-12
UKIRI
Kuanzia leo kila atakae jigeuza kwa sura yoyote nitamuona kwa Jina la Yesu.
Haimanishi kuwa mashetani wanaouwezo wa kutengeneza chura, au nyoka au fimbo ila tu waliweza kunuizia kitu kikageuka na kutimiza lengo. Malaika anaweza kufanya vile hata mashetani wanaweza kuvaa sura na maumbo ya kitu na kutimiza kusudi. Imeandikwa;

Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.2Wakoritho 11:14 

AINA NNE ZA MASHETANI
1. Majoka amabao ni roho ya uovu walioanguka kutoka mbinguni baada ya uasi. Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; Ufunuo 12;7
2. Mizimu. Haya ni mashetani waliotawala ukoo kwa muda mrefu.
3. Miungu. Ni mashetani waliopewa makafara kwa muda mrefu na wakapewa nguvu na kuwa miungu
4. Majini. Hawa nai mashetani wenye asili ya kiarabu.
Imeandikwa;
Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Ufunuo 16:13
Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza; Ufunuo 18:2
Nguvu kubwa ya mashetani ni ule uwezo wa kutowatambua. Wanapotoka ndani huwa wananuiza na kuvaa maumbo bandia. Wachawi nao huwa wanasikiliza kama umewatambua, wakiona umeona visivyo wanafurahi maana wanajua kuna biashara inaendelea na wamefanikiwa.
Ukiri.
Kuanzia leo lazima kila atakekuja kuniroga nitamuona kwa jina la Yesu.Kila aliyegeuza umbo naamuru nimuone katika umbo lake la siri.

Watu wengine wanajisikia kama wana misumari ndani ya miili yao lakini jambo amabalo hukulijua kama limetengenezwa an kugeuka kuwa kisu ndani ya miili yao. Ukiona nchi inayumbayumba lazima ujue kuna chanzo chake kiko katika ulimwengu wa roho. Ukishinda rohoni unaweza kuua kwa siraha isiyorasmi.

Yawezekana umeumwa sana na hujui namna ya kutatua tatizo ulilonalo.Imeandikwa;
Inawezekana, unajisikia hali mbaya hasa ya kumtukana mume wako, au mke wako lakini kwa akili zako huwezi kusema vile, lakini ukajikuta unasema vile. Kimsingi kuna viumbe wa rohoni wanakaa ndani yako ndo maana wakati mwingine unajikuta umeshatukana.
Inawezekana, unaona uso wako unaweka makeup, lakini sura iko kama babu, jambo usilolijua ni kuwa yuko aliyetumwa na kugeuka na kuwa babu.
MAOMBI
jini, joka, mzimu, aliyegeuka umbo na kuja kwangu, lazima nikuone katika jina la yesu.nina waamuru wapigwe katiak jina la yesu.Mimi ni askari naangusha ngome za balaa, ngome za mikosi, ngome za magonjwa katika jina la Yesu. Mimi nakataa kutawaliwa katika jina la yesu.
Kuanzia sasa roho yoyote iliyogeuka na kuwa balaa, talaka, mikosi, magonjwa, naivunja katika jina la yesu. Kwa jina la yesu kuanzia leo chochote kilichotumwa, nilichikinunua, nakiangamiza katika jin layesu. Kitu chochote, au roho yoyote, iliyondani ya nyumba yangu naivunja, na irudisha ilikotoka katika jina la Yesu.
Kwa jina la yesu,
2. UNAMFUMBA MTU ASIKUTAMBUE.
Katika sheria mbili za rohoni pili ni kukufumba usimtambue, na wewe ukiona unahisi ni vitu hivyo ulivyoviona kwa macho au katika ndoto. Akili ya mtu akifungwa mtu akiona hatambui kama ni wachawi au mashetani. Yawezeka kila ukilala na kuota ndoto ukiamka unaanza kusema uliyoyaota ambayo yako katika sura bandia. Inatakiwa uwafunge ili wasijifiche wakija uwatambuae katika jina la Yesu. Omba maombi haya kwa jina la Yesu. Maana imeandikwa Imeandikwa ;
Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya Yohana 14:13-14
MAOMBI
Katika jina la yesu namteketeza mtu yeyote aliyejigeuza sura ili anitese namfyeka katika jina la yesu.
Kila atakaekuja katika umbo lolote lazima nimjue katika jina la Yesu, ninawafunga wasinitambue kama nimewaona. Kuanzia leo naamka toka usingizi wa kiroho, na akili yangu iwaze kutawala, iwaze biashara katika jina la Yesu . Kuanzia leo naanza kutambua kazi yangu, nianze kuelewa kazi ya kufanya, biashara ya kufanya, katika jina la Yesu.

Nawashambulia mashetani wote katika jina la Yesu, mashetani walioshikiria familia yangu, kazi yangu, ndoa yangu, biashara yangu katika jina la Yesu nawaangamiza katika jina la Yesu. Nawaangamiza maadui wote katika jina la Yes. Natumia mamlaka aliyonipa Yesu nawafyeka wanaozuia kazi yangu nawafyeka wanaozuia ndoa yangu, nawafyeka wanaozuia huduma yangu, katika jina la Yesu. Nawashambulia kwa damu ya mwanakondoo.
Imeandikwa;
Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana. Isaya 54:17

Nawafyeka katika jina la Yesu, mtu yeyote aliyesimama kwenye njia zangu kunizuia nisifanikiwe, kuzuia nisisonge mbele kunizuia nisipate ajira, nafunga uwezo wako wa kujigeuza na kuwa balaa, nakujigeuza kuwa mikosi, kuwa matatizo ,kuwa mtego na balaa, nawashambulia katika jina la Yesu.
Naharibu uwezo wenu katika jina la Yesu, ng’oa madhabahu zenu katika jina la Yesu. Nawatiisha, na kata mamlaka zenu, kaila kiumbe kinachotumia mazira kuharibu maisha yangu nawashambulia katila jina la Yesu. Naaribu uweza wenu wote katika jina la Yesu.

Natangua yote uliyoyapanga katika jina la Yesu. Imeandikwa; yeye uyatangua mashauri ya wadanganyifu na mikono yao isipate kutimiza makusudi yao.

Kila vibarua wa shetani mnaovaa sura bandia nawaangamiza katika jina la Yesu, navunja kila laana ya familia iliyonipata kupitia viumbe wa rohoni mnaojibadilisha sura na kuniroga nawafyeka katika jina la Yesu.

Kila nguvu ya giza inayotawala nailaani katika jina la Yesu, kila balaa zinazotawala nazivunja katika jina la Yesu. Nakiri leo niko huru, kazi yangu iko huru katiaka jina la Yesu. AMEN
Inua mikono juu; na ukiri maneno haya kwa nguvu
Kila jini aliye ndani yangu uliyeingia ili mimi nisiolewe, ili uniletee balaa, imeandikwa lolote mtakalolifunga hapa duniani , litafungwa na mbinguni ewe jini uliyetumwa ofisini kutoka kijijini, nakuapisha dhihirika na ujulikane kwa jina la Yesu. Jini makata, jini wa hasira, jini wa mikosi, kila aliyerogwa kwa kuwekewa dawa kwenye tumbo la uzazi, kwenye maji ya kuoga, kwenye chakula, kwenye kitanda, kwenye nguo, kwenye damu wakati wa siku zangu naamuru moto ndani yangu ukuunguze na unitoke katika jina la Yesu.

AMEN.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.