WAIMBAJI WA KIGENI WAZIDI KUVUNJA REKODI NDANI YA JOYOUS CELEBRATION

Joyous Celebration Choir.
Waimbaji wanaotoka nje ya taifa la Afrika ya kusini wanaoimba ndani ya kundi maarufu kwasasa ndani na nje ya Afrika la Joyous Celebration ndio wameonekana kulitambulisha kundi hilo vyema na kuvunja rekodi kuliko waimbaji wazawa wa nchi hiyo.

Waimbaji ambao wametambulisha Joyous kimataifa ni mchungaji Agu Uchechukwu ama mwite Pastor
Pastor Uche.
Uche kupitia wimbo wake wa 'My God is good' unaimbwa takribani katika kila taifa duniani ikiwa pamoja na kuvunja rekodi ya kuwa wimbo wa kwanza wa Joyous kutazamwa zaidi ya mara millioni 2 kwasasa katika mtandao wa YouTube. Wimbo huu ndio pia umemtambulisha mwimbaji huyo kimataifa na kuwa mwimbaji anayeongoza kwa mialko kuliko mwimbaji yeyote wa kundi hilo.

Aidha wakati Uche ameshajitoa katika kundi hilo, mwimbaji mwingine kutoka nchini Zimbabwe kijana Mkhululi Bhebe ndiye anafuata nyayo za pastor Uche, tayari ameshavunja rekodi kwa nyimbo zake mbili Tambira na Itshokwadi kutazamwa zaidi ya mara millioni kwenye YouTube huku pia wimbo Namata katika album ya 17 umeshatazamwa na watazamaji zaidi ya laki tano, kama haitoshi wimbo mpya katika album ya 18 tayari umeshaanza kushika nafasi za juu katika mtandao huo.

Mkhululi Bhebhe.
Waimbaji hao pia wanashindana kwa nyimbo zao kusikilizwa zaidi katika mtandao wa muziki kama Spotify kuliko nyimbo nyingine za kundi hilo. Mkhululi pia amekuwa akialikwa zaidi kimataifa kuliko waimbaji wengine wa Joyous. Katika kuonyesha kwamba jambo hilo lipo, kiongozi wa kundi hilo Pastor Jabu Hlongwane aliwahi kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba anashangazwa kwanini nyimbo za Afrika ya kusini hazipigwi katika mataifa ya ulaya na Marekani licha kutegea sikio awapo nje ya nchi hizo.

             Itshokwadi wimbo namba 2 Mkhululi kuimba na Joyous Celebration DVD ya 16

                Overflow ni wimbo wa mwisho Pastor Uche kuimba na Joyous Celebration 16
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.