WORSHIP IN YOUR PRESENCE YASOGEZWA KUPISHA 'UKO HAPA' YA LISU

Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake walikuwa wanajishauri ni namna gani watajigawa siku ya Jumapili kwa ajili ya yaliyokuwa matamasha mawili makubwa, La kwanza likiwa la uzinduzi wa John Lisu, na la pili likiwa la Worship in your presence. Hatimaye sasa jibu limepatikana baada ya kuahirishwa kwa Worship in your presence hadi 25 December 2014 kupisha uzinduzi wa album ya mkongwe John Lisu.

Aidha haijafahamika zaidi mwanzo wa upangaji wa ratiba ni yupi alitangulia, lakini hatimaye mambo yote yako sawia. Mara kadhaa GK imemtafuta muandaaji wa Worship in your presence bila mafanikio, maana simu iliishia kuita tu.

Kwa sasa, njia zote kesho ni Diamond Jubilee, huku ukiweka sawa ratiba yako kwa ajili ya Krismasi, ambapo tayari kwa haraka haraka, kutakuwa na matukio mengi.

Lakini kabla ya kumaliza, Otkoba 6 2013 Uko Hapa live recording ndio ilifanyika CCC (bofya kuona), lakini tarehe 5 ya mwezi huo kwa mwaka 2014, tunahamia Diamond Jubilee kuikamilisha (tazama maandalizi). Labda ni mapema kuuliza, ila Oktoba 7 2015, huenda kukawa na jambo. GK itakuwepo, tukutane sote Diamond Jumapili hii.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.