YESU KUOKOA MITAA LEO HII ARUSHA

Kwa ufupi ikifahamika kama Y.O.M, ama kwa urefu wake; Yesu Okoa Mitaa, ndio jina la vuguvugu la injili kupitia vijana ambao hutumia nyimbo zinazoendana na rika la vijana ili kwenda nao sawa hadi kumpokea Yesu.

Ndani ya Kanisa la Heritage of Faith (HFCC) maeneo ya Silent Inn - nyuma ya Monor Hotel, ndipo ambapo tamasha la kusifu na kulitukuza jina la Mungu litakuwepo kuanziasaa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni. Kama uko mjini Arusha, basi karibu ujumuike na vijana wenzako (wazee wanakaribishwa pia :-) ) kama vile Rungu la Yesu, Mnene M, Apostle Bashando na wengineo wengi.

Tukutane hapo kuanzia saa nane mchana, Gospel Kitaa itakuwepo.Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.