YESU OKOA MITAA YAZINDULIWA KWA MATUMAINI ARUSHA

Jumamosi ya tarehe 26 imekuwa siku ya kipekee jijini Arusha, pale ambapo vuguvugu la kuwakusanya watenda kazi wenye nguvu (vijana) na kuwarudisha kwa Yesu  limezinduliwa rasmi, yaani Yesu Okoa Mitaa Project.

Tukio hili ambalo limekutanisha vijana wa rika mbalimbali kwenye Kanisa la Heritage of Faith lililopo Sakina, Silent Inn, limekuwa na mafanikio licha ya idadi ndogo ya watu kujitokeza kutokana na kutangazwa tu kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa musisi wa Yesu Okoa Mitaa, Rungu la Yesu, ameeleza kufurahishwa na vipaji ambavyo watu wa kaskazini wanavyo, na kuwatahadharisha wana Dar es Salaam ya kwamba pamoja na kutangulia kwao, wakae chonjo.

Aidha Rungu ameongeza ya kwamba kwa kuwa kuna uongozi wa YOM hapa Arusha, anategemea kusikia maendeleo zaidi na hata siku moja kuwa na kusanyiko kubwa zaidi.

Mmojawapo wa waratibu wa YOM Arusha, Mchungaji Barnabas Phillip, ameeleza kwa upande wake kwamba hili jambo litaendelea kukua na kukua, pengine hata siku moja wakiungana na wana t-shirt na jeans na hata zaidi na zaidi - huku akiwaasa wachungaji wenzake kuwapa nafasi ya kuhudu vijana makanisani, kwani ni nguvu tosha ya kuangusha ngome za mwovu shetani. Maneno ambayo hayapishani na wito alioutoa makamu mwenyekiti wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania kanda ya Kaskazini, Bw. Pokea Peter Kamata

Pamoja na kuimba na kuonyesha sanaa ya sarakasi vijana wametakiwa kuomba Mungu apatae kuwaendeleza na kufikia idadi kubwa zaidi ya wanakondoo waliopotea, na hata wale ambao hawajawahi kuwepo zizini.

Gospel Kitaa ambayo ilikuwepo mwanzo mwisho sanjari na wadau wengine, inatoa pongezi kwa hatua hii ya awali, kwani shuhuda nyingi zimesikika namna watu walivyobadilisha njia zao kupitia muziki wa gospel hip hop. Injili yastahili kuenezwa kwa njia tofauti tofauti, kutumia vipawa na uwezo tulionao.

Yawezekana hata wewe umekalia kipawa ambacho Mungu anataka ukitumie kufikia mamia ya watu, Mungu akuwezeshe kubadilika na kufanya jambo kwa ajili ya utukufu wake kwa Jina la Yesu. Amina.

Kilichojiri kwa uchache pale HFCC FIREPLACE

Mtoto Miriam Paul
step by step
Edson Zagalla


Bofya hapa kutazama picha zote...

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.