YNA AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME, MARA CLARA KUIGIZA UPYA KAMA YNA KWENYE THE PROMISE

Kaleb Hans Sotto aliyezaliwa juzi jumamosi
Mwigizaji nyota wa filamu na tamthilia nchini Ufilipino mwanadada Kristine Hermosa almaarufu kama Yna au Arabela majina aliyotumia tamthilia za The Promise pamoja na Timeless amejifungua mtoto wa kiume alfajiri ya jumamosi huko nchini kwao Ufilipino.

Kristine ambaye ameokoka pamoja na mumewe kijana Oyo Boy Sotto walikuwa na hamu kupata mtoto huyo wa kiume hasa baada ya kujaaliwa mtoto wa kike aitwaye Ondreas miaka mitatu iliyopita,
Binti wa Kristine akiwa anamshika mdogo wake.
huku pia wakiwa na mtoto mwingine wa kiume waliyemchukua kutoka kituo cha watoto yatima. Kupitia ujumbe alioweka kwenye instagram pamoja na Facebook mume wa Kristine amemshukuru Mungu kwa zawadi hiyo ya mtoto wa kiume waliyempa jina la Kaleb Hans Sotto.

Kujifungua kwa Kristine ni habari njema kwa mashabiki wake wanaomsubiri kwa hamu mwigizaji huyo ili arejee tena kwenye fani yake ya uigizaji, ingawa mwanadada huyo anayetambulishwa kama mmoja kati ya waigizaji warembo katika historia ya waigizaji wa Ufilipino, tayari alishasema anafurahia sana maisha yake ya sasa hususani watoto ambao amejaaliwa na Mungu, hivyo kipaumbele kwake kwasasa ni familia kwanza mengine baadaye.

Mume wa Kristine pamoja na watoto wao.
Wakati huohuo baada ya mwigizaji huyu kukataa kuigiza kwa upya tena tamthilia maarufu kuwahi kutokea kwenye medani ya uigizaji Ufilipino ya Pangako Sa'yo au The Promise, bado haijawekwa wazi nani atakayeigiza na Jericho Rosales ama Angelo ambaye amekubali kushiriki katika tamthilia hiyo ingawa hatashiriki kama mwigizaji mkuu bali wote walipewa ofa ya kuigiza kama wazazi kitendo alichoshauriwa Yna na mumewe kutokubali na kuachana na tamhilia hiyo.

Kristine na Jericho (Yna na Angelo ndani ya The Promise).
Wasanii wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya Yna na Angelo ni mwigizaji mkuu wa tamhilia ya Maria Clara aitwaye Kathryn Bernado aliyeigiza kama Maria katika tamthilia hiyo iliyowatoa wengi machozi lakini pia ikiwa imerudiwa upya kurekodiwa na chipukizi hao kwakuwa tamthilia yenyewe halisi ya Maria Clara ilionyeshwa kwa miaka mitano toka mwaka 1992 hadi mwaka 1997, na kurudiwa upya mwaka 2010.

Kutokana na mafanikio ya tamhilia hiyo ndipo binti huyo akishirikiana na mwigizaji wa kiume aitwaye Daniel ambao kifupisho chao huitwa (Kathaniel) kama ilivyo kwa Angelo na Yna kifupisho chao ni Echotin, ndio wamechaguliwa kuwa waigizaji wakuu wa marudio ya tamthilia hiyo ya The Promise, ingawa kuna kelele nyingi watu wakitaka kutorudiwa kurekodiwa kwa tamhilia hiyo ambayo imelitangaza vyema taifa lao la Ufilipino wakisema ikirudiwa itaharibiwa.

Kutokana na mawazo yanayotolewa na wengi nchini humo, imefikia kijana Jericho Rosales ambaye alioa hivi karibuni kuomba aondolewe kuigiza katika tamhilia hiyo ili kutoharibu sifa aliyojitengenezea na mwigizaji mwenzake walipoigiza tamthilia hiyo kwa mara kwanza, huku pia akipongeza wasanii waliochaguliwa kuigiza nafasi zao kwa upya.

Kathryn na Daniel wanaochukua nafasi ya Yna na Angelo kwenye marudio ya The Promise itakayoanza upya mwakani.
Chini ni moja ya kipande cha Yna na Angelo walipoigiza The Promise takribani miaka 12 iliyopita.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.