CHAGUO LA GK NI 'UPENDO' KUTOKA KATIKA DVD MPYA YA JOHN LISUKatika chaguo la GK jumapili ya leo tumekuchagulia wimbo 'Upendo' kutoka kwa nyota wa muziki wa injili nchini John Lisu, wimbo huu ambao ni marudio unapatikana katika DVD yake mpya kabisa iitwayo 'Uko Hapa' iliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salaam.

DVD hiyo ambayo ilirekodiwa live katika ukumbi wa  wa kanisa la  Assemblies of God City Christian Centre Upanga jijini Dar es salaam tayari imetokea kupendwa na wengi walionunua kazi hiyo. Basi sindikiza jumapili yako kwakutazama wimbo huu ambao tunatumaini utafanyika faraja katika maisha yako.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.