DR MYLES MUNROE NA MKEWE WAFARIKI KWA AJALI YA NDEGE

Marehemu Dr Myles Munroe na mkewe Bi Ruth Ann Munroe ©Forbes
Tasnia ya injili na hata ulimwengu mzima umezizima baada ya kupatikana kwa taarifa ya kufariki kwa mhubiri na mzungumzaji mashuhuri duniani, Dr. Myles Munroe pamoja na mkewe, Bi Ruth Ann Munroe, pamoja na watu wengine 7 kwenye tukio ambalo limeripotiwa kutokea tarehe 9 Novemba 2014 na kuthibitishwa leo tarehe 10 Novemba 2014.

Dr. Myles ambaye hivi karibuni alikuwa Afrika Mashariki, kwenye tukio la Africa Lets Worship (AFLEWO) lililofanyika jijini Nariobi na pia kuwepo kwenye jiji la Dar es Salaam, akinena na viongozi na wafanyanbiashara kabla ya kupanga ratiba ya kuwa nchini Burundi, alikuwa akielekea kwenye mkutano ulioandaliwa na taasisi yake ya Bahamas Faith Ministries ambapo kulikuwa na ratiba ya viongozi mbalimbali duniani ikiwemo kutoka Marekani.

Myles Munroe, ambaye pia ni mzungumzaji mshauri kwenye masuala ya biashara alikuwa kwenye ndege yake binafsi ambapo walikuwa wanakaribia kutua kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Bahama International Airport, ambao pia niuwanja binafsi na kisha kujigonga kwenye "crane", tukio lililopelekea kulipuka kwa ndege hiyo na kisha kuanguka chini.
GK itaendelea kuwaletea taarifa zaidi kwa kadri zinavyotufikia. Kwa hivi sasa, tunatoa pole kwa kila aliyeguswa kwa kifo hiki ambacho imekuwa ngumu kuamini, ni kama vile Munroe alikuja kuiaga Afrika.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.