JOYOUS KUFANYA ONYESHO NCHINI KENYA MWEZI UJAO, VIINGILIO VYATANGAZWA

Baadhi ya waimbaji wa Joyous wakiwa jukwaani hapo jana mjini Kimberly Afrika ya kusini katika onyesho lao.
Kundi la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini linatarajiwa kufanya tamasha mwezi ujao jijini Nairobi nchini Kenya. Taarifa hizo zimetolewa na kundi hilo kupitia ukurasa wake wa Facebook ikiwa ni kuwataarifu mashabiki wake kukaa mkao wa kura siku ya tarehe 14 mwezi ujao.

Onyesho hilo linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa kanisa la Christ Is The Answer Ministries (CITAM) NPC Karen valley road jijini Nairobi ambako kulifanyika Aflewo mwaka 2012, onyesho hilo tayari limepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa kundi hilo nchini Kenya ambao wameandika jumbe mbalimbali kwenye kichwa cha taarifa ya ujio wa kundi hilo nchini mwao na kutoa mapendekezo mbalimbali kuhusu waimbaji wapya na wazamani ambao wangependa kuwaona katika onyesho hilo.

Kiingilio katika onyesho hilo kimetajwa kwa watu wazima kulipa 2000 ya Kenya sawa na 38, 526 watoto 800 sawa na 15,410 na viti maalumu ni 3000 sawa na shilingi 57,789 za Kitanzania. Joyous inaendelea kupanua mipaka ya huduma yake baada ya kazi zake kupendwa katika kila nchi iliyopata nafasi kusikiliza nyimbo za kundi hilo, ambapo mpaka sasa limeshatembelea Zimbabwe, Ghana, Cameroon, Swaziland na nchi nyinginezo jirani na Afrika ya kusini.

Mmoja wa viongozi wa Joyous Celebration mchungaji Jabu Hlongwane katika mahojiano jijini London nchini Uingereza mwaka juzi alizungumzia uwezekano wa kundi hilo kufanya onyesho nchini Tanzania mwaka jana na tayari kwa wakati ule kundi hilo lilishatuma wawakilishi wake kupeleleza kama vigezo wanavyovihitaji ili kutembelea vipo. Kazi kwenu wapenzi wa Joyous mnaweza kujongea nchini Kenya taratibu kabisa kuliona kundi hilo.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.