NAMNA YA KUJIWEKEA AKIBA YA KUTOSHA KWA AJILI YA BAADAE

Faraja Naftal Mndeme.
GK Contributor.


1. Epuka Kutumia zaidi ya asilimia 15% ya kipato chako cha mwezi kwa ajili ya kulipa kodi ya nyumba. Hii ni kwa wale ambao wanajitegemea na wamepanga. Mara nyingi tunatumia fedha nyingi kwa ajili ya kulipia pango sababu ya status za sehemu fulani au ili tuonekane bora, na watu wa maana mbele za jamii. Ili kuweza kufikia malengo yako ya siku za usoni epuka sana kutumia zaidi ya asilimia 15% ya kipato chako kwa ajili ya kulipa pango. Jaribu kubalance kati ya asilimia 10 % - 15% ya kipato chako. Jaribu kutoka nje kidogo ya mji ambapo gharama za malipo ya nyumba ziko chini kwa kiasi fulani. Pia kwa wewe unayeanza kujitegemea itakusaidia zaidi.

2. Epuka kubadilisha badilisha wapenzi na kuanzisha mahusiano mapya mara kwa mara. Hakuna mtu ambaye hapendi kupendwa, lakini kiukweli kuna maisha zaidi ya mapenzi. Ni muhimu kuangalia kwa umakini swala la kuanzisha mahusiano mapya mara kwa mara. Hakuna mahusiano yasiyo na gharama. Gharama yake inaweza isiwe moja kwa moja lakini lazima kuna kiasi kikubwa cha matumizi ya fedha kitajumuishwa mwanzo wa mahusiano. Epuka pia kuwa na mahusiano yasiyokuwa na tija wala mwelekeo kwenye siku zako za usoni haswa katika swala zima la kifedha na ki-uchumi. Ukiona mahusiano yoyote yapo kama burudani ni bora uachane nayo. Kama una mpenzi mmoja usiongeze mwingine, baki na mmoja tu, inatosha.

3. Jaribu na jifunze kuhakikisha kila mwisho wa mwezi au katika kila fedha unayopata faida kwenye kipato chako unajiwekea akiba ya kiasi kisichopungua 10%. Kama utaweka zaidi ya hapo si vibaya. Lakini jaribu kufanya hivyo mara kwa mara na sehemu ya 10% isiguswe kwenye matumizi kabisa na wala isiwe kwenye mahesabu yako ya bajeti ya kila siku. Jenga utamaduni huu, itakusaidia kuweza kuwa na uhuru kwa sehemu kwenye fedha na kuweza kufikia malengo uliyojiwekea kwa muda mrefu na muda mfupi..

4. Hakikisha unapelekea kanisani 10% (Fungu la Kumi) kwa kila pato unalolipata kwenye maisha yako ya kila siku. Kwa wale wakristo na kwa wale ambao wana imani nyingine, hakikisha unafuata mfumo wa imani yako ya utoaji mara kwa mara ili kuweza kujipatia si tu baraka za Mungu, lakini pia kupata ulinzi wa kimapato kutoka kwa Muumba wako.

5. Fuata kanuni za afya. Mara nyingi tunaingia gharama zisizokuwa na msingi sababu ya kukiuka kanuni za ki-afya, na matokeo yake gharama za matibabu huingia kati na baadae tunaanza kulalamika. Mfano, unapoambiwa usinywe maji yasiyochemshwa, wewe unakunywa, matokeo yake mwisho wa siku utaugua tumbo, utaanza gharama za matibabu na kadhalika. Mara nyingi serikali muda mwingine hutoa chanjo za aina mbali mbali kwa ajili ya kutukinga dhidi ya magonjwa, lakini sisi wengine wajuaji tunagoma. Mfano, umeambiwa kanuni za kinywa ni kupiga mswaki mara mbili - then wewe fanya ...Siku unapougua utalala chini na utatumia gharama kubwa za matibabu ambazo zingeweza epukika.

E-mail: naki1419@gmail.com
+255719742559
God Bless Y’All

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.