SERIKALI KENYA YAPIGA MARUFUKU USAJILI WA MAKANISA NA MISIKITI MIPYA

Mtume Victor Kanyari wa huduma ya Salvation Healing Ministries Church iliyokumbwa na mtikisiko.
Mwanasheria mkuu wa Kenya amepiga marufuku na kuongeza sheria kali ya kutoruhusu usajili wa makanisa ama misikiti mipya baada ya kugundulika baadhi ya watumishi hufanya miujiza ya uongo ili kuvuta waumini kwenye nyumba zao za ibada kwa lengo la kujiongezea kipato.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa umoja wa makanisa ya kiinjilisti nchini humo Askofu Mark Kariuki amesema linapokuja suala la imani watu wapo tayari kufa kulinda imani yao nayeye pamoja na wenzake watasimama kidete na kanisa na kuwataka wakristo wote kuwaunga mkono na kusimama pamoja nao katika hilo.

Askofu Kariuki na mkewe.
Siri ya kuwepo miujiza bandia imekuja baada ya kituo maarufu cha runinga nchini humo cha KTN kupitia moja ya habari zake za kipelelezi kupitia kipindi cha 'Inside story investigative' kilichopewa jina la 'Prayer Predators' kimefichua siri ya mchungaji aitwaye Victor Kanyari wa huduma ya 'Salvation Healing Ministry church' ya jijini Nairobi anayerusha matangazo yake kwenye runinga amekuwa akitoa shuhuda na miujiza bandia kuvutia waumini ambao wamekuwa wakimpatia pesa.

Taarifa ya kituo hicho imedai mchungaji Kanyari amekuwa akiwataka watu kutuma michango yao kwa njia ya simu kabla hawajafanyiwa maombi. Askofu Kariuki ameelezea hisia zake kuhusu vizuizi, amesema 'nyanya moja inapooza haimaanishi zote zimeoza, na ikiwa waumini watakwenda kwa mtumishi huyo inamaana makanisa mengine watapata matatizo, alisema askofu Kariuki alipozungumza na Daily Nation la Kenya.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.