SHANGWE ZA GK NI HARUSI YA MWIMBAJI WA INJILI NCHINI PIA NI BLOGGER

Pius na Catherine Senyagwa wakienda sawa.
Shangwe za GK jumamosi ya leo ni kwa muimbaji wa nyimbo za injili nchini pia mmiliki wa blog ya Iyelele team kijana Pius Senyagwa ambaye siku ya November mosi mwaka huu alifunga ndoa na mpenzi wake Catherine katika kanisa Anglikana Ubungo jijini Dar es salaam na kufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa Ubungo Riverside jijini Dar es salaam.

Pius kabla hajaanza kuimba kama mwimbaji binafsi pia anashiriki na kwaya kongwe ya Uvuke ya kanisa kuu Anglikana mkoani Dodoma na unaweza kumuona vyema kwenye DVD ya kwaya hiyo iitwayo 'Lisikieni Neno' ambapo Pius ameanzisha wimbo uitwao 'Ukimwi' na nyinginezo.

Team GK inawapongeza maharusi kwa hatua yao mpya ya maisha ya wawili, Mungu aliyeanzisha jambo hili katikati yao basi yeye mwenyewe akapate kuwafikisha salama katika maisha yenu ya ndoa.   KAMA HUWAFAHAMU UVUKE CHOIR BASI TAZAMA VIDEO HII KWA UFUPI


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.