SIMBA WA YUDA AUNGURUMA KILOSA, WATU 30 WATOKA KWENYE UISLAMU, MSAADA WAHITAJIKA

Yesu amejidhihirisha katika mkutano wa injili wa wiki moja uliomalizika jana huko kijiji cha Kidogo bass kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro ambako watu 30 waliyakabidhi maisha yao kwa Kristo wakiachana na dini yao ya kiislamu, huku pia mmoja wa viongozi wa dini hiyo akifariki dunia siku ya jumamosi ikiwa siku moja tu baada ya kuamuru kusitishwa kwa mkutano huo akidai unawapigia makelele.

Mkutano huo ulioanza siku ya jumapili iliyopita na kuisha jana muhubiri alikuwa ndugu Lonas Kihwele aliyealikwa na rafiki ambaye ndiye mchungaji wa kanisa dogo la Tanzania Assemblies of God (T.A.G) lenye waumini wanne tu pia hali ya kanisa ikiwa mbaya huku kukiwa na zaidi ya misikiti nane kijijini hapo.

Baada ya mkutano huo watu wengi wamempokea Kristo, ambapo mtumishi huyo ameomba msaada wa mabati 25 ili aweze kuweka vyema kanisa hilo, hasa kipindi hiki cha mvua wilayani humo.
Muhubiri wa mkutano huo mtumishi Lonas Kihwele amezungumzia kuhusu kiongozi wa kiislamu aliyefariki baada ya kutaka mkutano huo kufungwa kwa madai unawapigia kelele
"Tulipokuwa tunaendelea na mkutano hapa siku ya ljumaa kiongozi mmoja wa msikiti alikuja na kutwambia tufunge mkutano tunawapigia kelele, Mungu alitwambia vita ni yangu hubirini jumamosi mtu huyo aliaga dunia alfajiri, Yesu ametukuka sana ndani ya kijiji hiki".
Kwa mawasiliano moja kwa moja na mchungaji huyo ili kumpatia msaada wa mabati kutengeneza kanisa hilo mpigie kwa simu namba 0685 863 454


Lonas Kihwele akihubiri mkutanoni hapo.
Baadhi ya watu waliofika moja siku za mkutano.
Lonas akihubiri. 
Watoto na wazazi wao wakiwa mbele katika mkutano huo.
Mchungaji akiwa ndani ya kanisa lake.
Lonas akiwa amepiga picha nje ya kanisa hilo.
Msaada unahitajika kuliweka kanisa hili katika hali nzuri ili kuvuta wengine waje kwa Yesu, namna ya kusaidia namba iko mwanzoni mwa habari hii.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.