SIO KILA ANAYEKUKOSOA NI ADUI

Na Faraja Naftal Mndeme
GK Contributor.

©Freetins
Kila mwanadamu ana namna alivyolelewa na alivyokuzwa, lakini pia kuna namna anavyochukua hatua mbali mbali katika kujifunza mambo kadha wa kadha ili kuleta faidi iliyo na tija kwake binafsi na kwa wanajamii wanaomzunguka.

Kwa asili binadamu hupenda kusifiwa na kupongezwa kwenye kila jambo ambalo anafanya lakini kiukweli si kila jambo ambalo tunalifanya linakuwa katika usawa wakuleta matokeo yaliyotarajiwa kwenye mambo kadha wa kadha. Kulingana na mfumo wa ujumvi ambao huwa mara nyingi watu wengi tumejiwekea kwenye maisha yetu tumeshindwa kujifunza mambo kadha wa kadha na inapotokea mtu akakosoa juu ya kile unachofanya mara nyingi huwa tunajenga dhana ya uadui katika vile ambavyo tunakosolewa. Je kila anayekukosoa anafaidika na nini kwako? Je kila anayekusifia hata unapoboronga anafaidika nini kwako? Ni maswali madogo lakini yanaweza kukuvusha na kuweza kukusaidia kuweza kujifunza zaidi.

Unapokubali kukosolewa mara nyingi unapata muda wa kuweza kujifunza vitu kadha wa kadha kutoka kwa wengine. Hakuna aliyezaliwa akijua vitu vyote, lakini kuna watu ambao huenda wana mtazamo mpana zaidi na mafikirio bora zaidi ambayo yanaweza kukufanya usonge mbele kwa haraka zaidi kuliko pale ulipo na pia hata kasi uliopaa nayo. Mara nyingi tumepoteza kujifunza na kupata hatua mpya zaidi katika kila tunalolifanya sababu tangu mwanzo tumejijengea dhana kwamba kila tunachofanya ni sahihi lakini kiukweli muda mwingine hatuko sahihi. Ni vyema kupenda kukosolewa sababu itakufanya ujifunze zaidi na kuweza kukufanya uwe mtu bora zaidi.

Unapokubali kukosolewa unapata kuongeza busara na ufahamu mpya kichwani mwako. Unapopenda kukosolewa pia utapenda kupata maonyo kadha wa kadha juu ya maamuzi mbali mbali kwenye maisha ambayo muda mwingine yangekuletea madhara bila ya wewe mwenye kujua katika siku za usoni. Kizazi chetu mara nyingi tukionywa kwa namna ya kukosolewa hatupendi na mara nyingi tunaona wanaotukosoa si bora kama sisi ili hali muda mwingine wao huwa bora kuliko sisi kwenye mambo kadha wa kadha. Unapopenda kuwasikiliza wengine hata wanapokukosoa inakujengea nidhamu ya kuweza kufikiria vyema zaidi kabla ya kufanya maamuzi mbali mbali.

Unapokubali kukosolewa pia jifunze kukaa kimiya tena kwa umakini ili uweze kujifunza zaidi na zaidi. Mara nyingi huwa tunajifunza kusikiliza ili tuweze kujibu kile tunachoambiwa lakini hatupendi kusikiliza kwa utulivu na ukimya ili tuweze kujifunza. Unapokosolewa na kurekebishwa faidi ni ya kwako binafsi na unapokuwa na tabia ya kujibu au kuongea ongea wakati unapokosolewa mara nyingi unajenga tabia kwa watu ambayo si njema. Hata iwapo ikatokea umefanya kitu ambacho si sahihi au umekosea watu wataogopa kukaripia au kukurekebisha sababu watanajua tabia yako na hapa ndipo utakapoachwa hata uharibifu na uangamivu ukufikie mwenyewe binafsi.

Ukiona mtu amefikia mafanikio kwenye nyanja fulani tambua kwamba kuna mahali alikosea na akakubali kukosolewa kwenye jambo husika na ndipo alipokaa chini na kufanyia kazi yale aliyokosolewa  na hatimaye akafanyika kuwa bora zaidi kwenye jambo husika. Kizazi chetu mara nyingi ukikimkosoa mtu utasikia unaitwa “HATER” lakini ki-ukweli hata mtu asingekukosoa yeye hangefaidika na chochote kutoka kwako anapokukosoa maana yake anamini unaweza kuwa bora zaidi ya hapo ulipo na unaweza kufanya katika kiwango cha juu zaidi kwenye mais vrtha yako.

Kila unapokosolewa chukulia jambo husika katika mtazamo chanya badala ya kuchukulia jambo husika katika mtazamo hasi, Ukichukulia kila jambo unalokosolewa kwenye mtazamo hasi utajenga uadui na watu wengi ambao haina ulazima. Unapokosolewa chukua kila ulichokosolewa kwa upole na unyenyekevu na kisha nenda kafanyie kazi, ukiona kina kufaa chukua endelea nacho na ukiona hakikufani unachana nacho.

“Sio Kila Anaye Kukosoa ni Adui”

E-mail:naki1419@gmail.com
+255719742559

God Bless Y’All

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.