SOMO: BARAKA ZA MUNGU - KING SAMBARAKA YA MUNGU
Bwana Yesu apewe sifa ndugu zangu katika Bwana.

Mithali 10:22 inasema Baraka ya Bwana hutajirisha,
Wala hachanganyi huzuni nayo.

Kuna baraka ambayo hata Mungu hawezi kuigeuza, Baraka ambayo haiwezi kuwa laana na wewe unaweza kuipata kwenye kitabu cha Mwanzo 22:1-18 Mungu alisema Na Abraham kumtoa Isaka kuwa Sadaka ,Abraham alitii Na Mungu mwenye Nguvu ikabidi amtoe kondoo Kwa ajili yake,wakati huo Mungu akasema,Abraham,Kwa sababu umefanya hivi Kwa ajili yangu,Nimeapa,kukubariki nitakubari,kukuongeza nitakuongeza uzao wako,Mungu akasema,Nimeapa,Baraka ambazo nimekubariki uwezi badilisha,

Mungu anaweza kufanya Kama alivyoamua kufanya,anaweza kubariki Mtu yeyote Kama atakavyo,anaweza kubariki mdogo kuliko mkubwa,Yeye ni Mungu,chochote anachofanya anafanya Kulingana Na maamuzi yake,

Mithali 26:2 Kadhalika laana I siyo Na sababu haimpati Mtu,
Kwa maana nyingine Mungu hawezi kukulaani pasipo Na sababu,lazima kuwepo Na sababu kabla Mungu ajatamka,Kwa namna nyingine Baraka pasipo sababu haiwezi kuja,
Torati 28:1-2 itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana Mungu wako Kwa Bidii,kutunza nakuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo Leo,ndipo Bwana Mungu wako atakaokutukuza juu ya Mataifa yote ya duniani.Inaweka wazi
Amesema,Baraka zitakufuata,

Mungu anafanya kazi zake Kwa principles.Torati 11:27-28 inasema Kama ukimtii Mungu,utapokea Baraka lakini usipomtii Mungu laana itakujia,
Mungu amekupa uchaguzi je,unataka Baraka au unataka laana?
Torati 30:19 nazishuhudiza mbingu Na nchi hivi Leo,kuwa nimekuwekea mbele yako Uzima Na Mauti,Baraka Na laana,basi chagua uzima ili uwe hai,wewe Na uzao wako.
Malaki 3:6-10 Mungu akasema watoto wangu Israel niwapendao kwanini mnaogopa kwanini mnateseka akawambia mkochini ya laana Kwa sababu mmeniibia Mimi Sadaka Na zaka,
Neno la Mungu liko wazi.
Baraka za Bwana ziko nyumbani mwa mwenye haki Na laana ya Bwana iko nyumbani mwa muovu.
Unataka nini Baraka au laana?

King Sam
Kama unataka niwasiliane na wewe kwenye simu namba yangu hii hapa +447903180067
Namba ya whatsapp hii +447977225185
Ubarikiwe na Yesu

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.