SOMO: KILA HATUA MPYA INALETA VITA VIPYA

©wikipedia
Wakati Mungu Anapotangaza Kwamba, "HUYU NI MWANANGU MPENDWA NINAYEPNDEZWA NAYE" Hapo hapo Ndipo Shetani Anapokuja NA JARIBU Akisema, "IKIWA WEWE NI MWANA WA MUNGU..." ZINGATIA: 1.Pale Mungu Anapokupa Mme/ Mke si wakati wa kushangilia na kulala usingizi baada ya maombi ya kuomba MME/ MKE MWEMA... Bali ni wakati wa kujipanga kwa MAJARIBU NA VITA KUBWA Ya KULINDA NDOA YAKO Pale Adui Atakapokuja Akisema, "IKIWA HUYU NI MMEO/ MKEO TOKA KWA BWANA; MBONA ANA A, B, C, D... SI MTU SAHIHI UMEKOSEA WEWE... ACHANA NAYE, UMEKOSEA..."

2.Pale Mungu Atakapokupa NAFASI YA KIELIMU: Si wakati wa kushangilia kwa kupata hiyo nafasi bali ni wakati wa KUOMBA SANA Maana Adui Atakuja Na MASOMO MAGUMU [Au MENGI], Atakuja Na WALIMU WASIOELEWEKA NA WASIO NA UTU, Atakuja na Mbinu Ya KUVURUGA UTAWALA AMA UONGOZI Ili UYUMBE NA KUKWAMA... Hili Ukiona Haya UPATE SHAKA Na Kuanza Kusema "SIDHANI KAMA NI MAPENZI YA MUNGU, SIDHANI KAMA NI MPANGO WA MUNGU... NADHANI SIKO MAHALI SAHIHI... NA MENGINEYO MENGI..." Kisha Unapoteza MORALI NA NGUVU YAKO YA NDANI YA KUENDELEA MBELE NA KUSHINDWA!!

3.Ndivyo Ilivyo kwa WANAOPATA KAZI, WANAOANZISHA BIASHARA ZAO, NA WANAOFANYA CHOCHOTE AMBACHO MUNGU ALIWAFUNGULIA MLANGO... Mara tu UKIKIPATA Na adui naye anakuja Na MAJARIBU Ya KUKUANGUSHA TOKA KWENYE HICHO... Usipojua Kwamba HATUA MPYA INALETA MAADUI WAPYA [WA KIROHO NA KIMWILI] Hakika HAUTAWEZA KUFANIKIWA HAPA DUNIANI.

"New Levels Brings New Devils" Benny Hinn Kila HATUA MPYA Inataka MAOMBI YA NGUVU Kuliko HATUA ILIYOPITA, Yesu Anajua Hili Naye Anatutahadharisha Akisema "SHIKA SANA ULICHONACHO... ASIJE MTU AKAKUNYANGANYA" Huyu Mtu Anaitwa Shetani, ANAZUNGUKA HUKU NA HUKO AKITAFUTA NAMNA YA KUKUNYANGANYA HICHO ULICHOPEWA NA MUNGU TAYARI. 

KESHENI MKIOMBA, MAANA HAMJUI SAA ATAKAYOKUJA MWIZI. "Laiti Mwenye Nyumba Angelijua Saa Atakayokuja Mwizi, Angelikesha Na Asingelala" Na HAUWEZI KUKESHA KWA AKILI YAKO "BWANA ASIPOULINDA MJI, WALINDAO WAKESHA BURE" Lazima Ujizoeze Kuombea KILA KITU Ambacho Unajua MUNGU Amekupa Maishani... WOKOVU, AFYA, MALI, KAZI, MME/ MKE, WATOTO, HUDUMA Nakadhalika... Ukikipata tu, Adui Anakuja KUSUMBUA. 

Mwl Dickson .Cornel .Kabigumila
+255 655 466 675 (Kupiga, text, Whatsapp na viber).

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.