SOMO: KIWANGO CHA UFALME WAKO KINATEGEMEA KIASI CHA AMANI YAKO

©Soothing Pictures Blog
HAUWEZI KUTENGANISHA UFALME ULIONAO KATIKA KRISTO YESU NA AMANI!

Sisi sote, wake kwa waume kama tujuavyo, ndani yetu mungu ametuumbia asili ya ufalme tangu mwanzo, ili tumilki na kutawala hapa duniani kwa niaba ya serikali ya mbinguni!

Kubwa zaidi, Kristo Yesu alitununua msalabani na kutuingiza kwenye Ufalme wa Mungu akiwa na kusudi moja kuu la kutufanya makuhani na wafalme tutakaomilki juu ya ...NCHI Kwa niaba ya serikali ya mbinguni (1 Wakorintho 4:1-2, Ufunuo 5:9-11).

Na kama sisi ni wafalme tulioko duniani kuiwakilisha serikali ya Mungu aliye hai, tunamiliki na kutawala katika maeneo yote ya maisha kwa kanuni na mfumo uleule aliokuwa nao Mfalme wa Mfalme, Yesu Kristo!

Ukisoma kwenye kitabu cha Isaya 9:6-7, tunaona kati ya 'Majina' anayoitwa Yesu ni "Mfalme wa Amani"

Hii ina maana kuwa kumilki na kutawala kwa Yesu kulikuwa kumefungwa katika kiwango cha amani aliyokuwa nayo!

Yesu kama Mfalme wetu sisi wafalme wengine katika Ufalme wa Mungu aliweza kumilki na kutawala alipokuwa hapa duniani katika mwili kwa sababu ya amani yake.... Hii ni kwa sababu ufalme wa Mungu ni "furaha, amani na haki katika Roho wa Mungu" (Warumi 14:17).

Somo la kujifunza

Kama Yesu mwenyewe anaitwa Mfalme wa Amani na alihitaji amani ili aweze kutawala na kumilki duniani, basi kutakuwa na siri kwenye amani.

Ayubu 22:21, "mjue sana mungu ili uwe na amani; ndipo mema yatakapokujia"
Hapa tunajifunza kitu cha muhimu sana kuwa kiwango chako cha kumilki na kutawala, na pia kuyapata mema na kuyafanya yatujie, kunategemea kiwango chetu cha amani!
Ukiwa na amani ya moyo na akili ndipo uwezapo kuwaza na kufanya mambo makubwa yanayokupa heshima kama mfalme katika kizazi chako!

Hii ndiyo sababu iliyomfanya Yesu atupatie "Amani yake" ili tuweze kumiliki na kutawala katika "kiwango na ubora kama wake"... BWANA Yesu anasema, "Amani yangu nawapa, niwapavyo mimi ni tofauti na ulimwengu uwapavyo" (Yohana 14:27).
 
Kama wafalme tulioko duniani kwa niaba ya ufalme wa Mungu hatutafurahia viwango vya juu vya ubora katika kumilki na kutawala kwetu kama hatutakuwa na bidii kuitafuta amani na kuitunza ndani ya mioyo yetu na akili zetu pia ili kuweza kuleta mapinduzi na maendeleo ambayo dunia haijawahi ona!

"MTU MBAYA NA AACHE NJIA ZAKE, NA AMRUDIE MUNGU NAYE ATAJENGWA, AITAFUTE AMANI NA AIFUATIE"


Wako Katika Kristo Yesu,
Mfalme, Mwl D.C.K
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.