SOMO: VIFUNGO VYA MAPEPO HUSIMAMA KAMA VIZUIZI KATIKA KUIFANYA KAZI YA BWANABwana Yesu asifiwe…

Awali ya yote napenda nianze kwa kukuelezea maana halisi ya ” mapepo “kibiblia.

Mapepo ni roho kamili ya shetani itendayo kazi yake kinyume na kazi ya MUNGU.roho ya yule muovu ni roho kamili maana ipo hata sasa ikitenda kazi kwa wana wa kuasi.

” Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;

ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ” Waefeso 2:1-2

~ Ili kazi itendeke basi nguvu inahitajika,maana kazi ni matokeo ya nguvu iliyo ndani ya kitu au mtu, au jambo fulani. Hivyo kama mapepo yanatenda kazi basi ni dhahili kabisa ipo nguvu ndani yao.

Biblia inatuhakikishia kwamba mapepo ni roho kamili ya yule muovu,maana twasoma;

” Na ndani ya sinagogi mlikuwa na mtu mwenye roho ya pepo mchafu, akalia kwa sauti kuu, ” Luka 4:33.

Tukihitaji kushindana na nguvu za mapepo,basi ni ukweli tutakuwa tunashindana ni ile roho ya shetani,na ikiwa tunahitaji kuwashinda basi tukubali kwamba ni lazima tuwe watu wa rohoni sana tukilitumia jina la Yesu maana ndilo jina lenye uwezo na uweza.

Vifungo hivi vya nguvu ya giza husimama kumzuia mtu asifanye mapenzi ya MUNGU.

Mtumishi Gasper Madumla pamoja na Mch. Eliya wakiwafanyia maombi watu.

Mfano mdogo tu ni huu;

Yamkini mtu siku ya jumapili alihitajika awepo kanisani akihudumu na kusifu pia,lakini kutokana na kufungwa na nguvu ya giza,mtu huyo ujikuta akielekea bar,au gesti house. Au utakuta mtu alihitajika awepo nyumbani mwa Bwana katika maombi,lakini hujikuta akielekea katika ugomvi na mwenzake. Yote haya huja kwa sababu ipo nguvu itendayo kazi ndani ya watu wa namna hii,nguvu ya namna hii ni vifungo visimamavyo kama ukuta kumzuia mtu kuitenda kazi ya Bwana MUNGU.

Siku zote roho hizi za nguvu ya giza,hazina kweli ndani yao maana baba yao ni muongo tangia zamani (Yoh.8:44). Biblia inatueleza vizuri hapa;

” Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; ” 1 Timotheo 4:1

Kumbuka,


Mtumishi Gasper Madumla pamoja na Mch. Eliya wakiwafanyia maombi watu.

Ninakuambia hivi,vifungo vya mapepo husimama kama ukuta kumzuilia mtu kufanya huduma ya Bwana Mungu. Sasa na hapa yupo mtu aliyefungwa muda mlefu hata kushindwa kuifanya kazi ya Bwana,naye si mwingine bali tunamsoma habari zake kupitia kitabu cha Marko 5:1-20.

Ngoja tusome kidogo habari hii;

” Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;

makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; ” Marko 5:2-3

◇ Ngambo ya nchi ya Wagerasi ilikuwa ni sehemu ambayo inakadiliwa kuwepo na watu wengi wa mataifa,na ndipo inaonekana palipokuwa ni makazi ya pepo wachafu,sababu hata ukisoma hapo chini kidogo katika Marko 5:9-10, utaona mapepo wachafu wakimsihi Bwana Yesu wasipelekwe mbali na nchi ile,imeandikwa;

” Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.

Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile. “

Lakini pia tunajifunza jambo jingine mara tu baada ya mapepo hayo kumtoka mtu yule, wakawaingia nguruwe. Nguruwe hawakuona faida ya kuishi na pepo wachafu, wakaamua wajitumbukize baharini wafe,na wakafa nguruwe elfu mbili. Kumbe hakuna faida yoyote ya kuishi na mapepo,ikiwa nguruwe walikataa kuishi na mapepo sembuse wewe!

◇ Nawe usikubali kuteswa na nguvu za mapepo,nenda ukaombewe na hizo nguvu zipate kukuachia,inawezekana kuishi pasipo vifungo vya mapepo,maana Yesu U hai kwa ajili yako.


Mtumishi Eliya wa huduma ya Bible restoration church-mtoni kijichi,Dar,akimfungua mama kwa uweza wa jina la Yesu Kristo wa Nazareti.

◇ Mtu huyu alikuwa amefungwa na mapepo wachafu kiasi kwamba hata makao yake hayakuwa nyumbani bali makabulini tena akajikata kata kwa mawe,kwa kifupi ni sawa na kusema kwamba mtu huyu alikuwa ameshindikanika kwa kamba za kibinadamu,bali Yesu tu pekee ndio anaweza.

Tazama sasa katika mstari wa 20 ( Marko 5:20) Imeandikwa;

” Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu. “

◇ Mapepo yalimchelewesha mtu huyu ambaye kumbe alikuwa ni muhubiri.

Tazama,vifungo vya mapepo vilivyomzuia mtu kutokuifanya kazi ya kuhubiri,hatimaye alikaa makaburini kama vile hakuwa muhubiri.

Hivyo ndivyo vifungo vya mapepo wachafu vinavyowafunga watu hata karama zao kushindwa kuonekana.

Ukiwa msomaji mzuri wa Biblia utaona kuwa wako baadhi ya watu waliofunguliwa na Bwana Yesu,na mara baada tu ya ukombozi,au uponyaji wao,utawaona wakimfuata Bwana Yesu. Mfano mzuri ni Bartimayo aliyekuwa kipofu,imeandikwa;

“Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.” Marko 10:52

Lakini hali ilikuwa ni tofauti kabisa kwa mtu huyu aliyekuwa na jeshi la mapepo maana mara tu baada ya ukombozi wa kufunguliwa katika vifungo vya pepo wachafu,tunamuona akitumwa aende DEKAPOLI kuhubiri injili juu ya mambo ambayo Yesu alimtendea. Mtu huyu hakumfuata Bwana Yesu kama Bartimayo alivyofanya na wengine walivyofanya,bali yeye alikwenda kuhubiri.

Kwa lugha nyingine ni kwamba mtu huyu alikwenda kuhubiri katika miji kumi,maana neno ” Deka” lina maana ya kumi,na ” poli” ni miji,hivyo Dekapoli ni miji kumi. Hivyo mtu huyu akaanza kuhubiri yaani kuifanya kazi ya Bwana. Kumbuka jinsi vifungo vya mapepo vilivyosimama kumzuia mtu huyu hata asiweze kujia kwamba ipo siku atahubiri.

Sijui hali ikoje kwako,!

Maana siku ya leo wapo watu ambao walitakiwa wawe wahubiri wakubwa,lakini wanacheleweshwa na vifungo vya mapepo,

Tena,nami nimeona karama za watu zikifukiwa na nguvu ya vifungo vya pepo wachafu,yaani wapo watu ambao wana karama lakini karama hizo hazitendi kazi sababu ya vifungo vya mapepo kwamba watu hao bado hawajampa Yesu maisha yao,hawajaokoka. Hivyo shetani hugandamiza karama zao,yamkini walistahili wawe waimbaji wa nyimbo za injili,likini leo ni wacheza dansa!

Mtumishi Eliya wa huduma ya Bible restoration church-mtoni kijichi,Dar,akimfungua mama kwa uweza wa jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
~ Milango ipo wazi kabisa ya kuombewa ili ufunguliwe kutoka katika hizo nguvu za giza zilizokushika,na kuokoka. Sasa waweza kunipigia kwa namba yangu hii hapa chini ili tufanye maombi pamoja,ili Bwana Yesu akufungue kama alivyomfungua huyo aliyekuwa na mapepo katika ngambo ya nchi ya Wagerasi. Piga sasa;

Mtumishi Gasper Madumla


Simu:    0655-11 11 49.

UBARIKIWE.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.