TAMASHA LA UPENDO KWA MAMA LAIVA, MAMBO YOTE JUMAPILI STADIUM ARUSHA


Hatimaye maandalizi ya tamasha la Upendo kwa Mama ambalo litafanyika Jumapili tarehe 16 Novemba jijini Arusha, yanaendelea vema huku mambo yote yakionekana kwenda sawia, GK Imefahamu. Tamasha hilo ambalo linarudiwa kutokana na lile la mara ya kwanza la tarehe 2 Novemba kutofanikiwa kwa ukamilifu kutokana na mvua kubwa iliyoanza kunyesha wakati ratiba ikiendelea, hali iliyolazimu kuvinusuru vyombo visipate kuharibika.

Hadi hivi sasa kuna waimbaji zaidi ya 5 ambao wameshafika kutoka nje ya Arusha, huku mwanamama Upendo Nkone akitua Jumamosi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, wakati Christina Shusho atakuwa akipokelewa kwenye mpaka wa Tarakea jijini mkoani Kilimanjaro, akitokea nchini Kenya. Kwa upande wa Arusha, wapo waimbaji zaidi ya 25 ambapo wameshakamilisha taratibu zote za kushiriki kwenye tamasha hilo.

Upendo kwa Mama ndio hiyo imewadia, kuja kuhamasisha upya fikra zetu na mitazamo hasi ambayo imekuwa miongoni mwetu kwamba wanawake ni wadhaifu na hawawezi kitu chochote, ijapokuwa ni mama ndiyo mwenye jukumu la kuisimamisha nyumba yake kwa uimara, akiwa na jukumu si tu la kulea watoto, bali pia hata kumlea baba.

Nuru na intaangaza
"Kama ambavyo inahitaji mtu mwenye nguvu kuja kusukuma gari lako linapokwama, ndivyo alivyo mama, ana nguvu ya kusukuma gari lolote ambalo limeharibika kwenye maisha yetu" Anaeleza mratibu wa tamasha la Upendo kwa Mama, Mhandisi Charles Mkundi.

Bado masaa machache hadi kutimu saa sita mchana ambapo huduma itakuwa imeanza tayari, muimbaji wa kwanza akipanda jukwaani.na kwa uchache tu watakaopanda jukwaani kuungana na Upendo Nkone na Christina Shusho ni pamoja na Hellen Kijazi, Mess Jacob Chengula, Manesa Sanga, Rebecca Magaba, Emanuel Mwaitege na wengineo wengi, ikiwemo kutoka nyumbani, Arusha ambao wakoza zaidiya 30.

GK ambayo imekuwa ikifuatilia kwa karibu kinachoendelea upande wa waandaaji, imeshuhudia idara mbalimbali zikiwasilisha ripoti na tathmini ya maandalizi kwa namna ambavyo wamejipanga kuhakikisha kwamba ratiba inaenda sawa, huku ikidhihirika kwamba maombi ndio yanayowabeba.

Tukutane uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume kuanzia saa sita mchana ambapo ratiba ndio ikianza rasmi, GK itakuwepo.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.