UPENDO KWA MAMA NDANI YA JIJI LA MOSHI, CHUO KIKUU CHA USHIRIKA.

Mara baada ya wakazi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake kuzindua tamasha la Upendo kwa Mama ambalo limefanyika tarehe 16 Novemba, Wakazi wa JIji la Moshi na vitongoji vyake watapata wasaa wa kukusanyika pamoja kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MUCO) kuanzia saa sita mchana hadi jioni ambapo waimbaji wakongwe ikiwemo Ambwene Mwasongwe, Upendo Nkone, na Christina Shusho watakuwepo kuhudumu siku hiyo.

Sanjari nao watakuwepo pia waimbaji kadhaa kutoka Arusha, bila kusahau wenyeji kutoka mkoa wa Kilimanjaro, ambapo hadi sasa uratibu kati ya kamatiya maandalizi ya Upendo kwa Mama na wadau wa mkoa wa Kilimanjaro yanaenda vema.

GK mbayo imeshriki kwenye baadhi ya vikao vya maandalili, imeshuhudia kila idara ikiwasilisha ripoti kulingana na majukumu ambayo iliwapewa, kuashiria kwamba kila kitu kinakuwa sawia.

Tarehe 30 Novemba 2014 ndio siku yenyewe, tukutane MUCO.

Tazama namna wimbo maarufu wa mama ulivyoimbwa. (reliving the moments.)

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.