UWEZO WA KIFALME MABEGANI UNAVYOTUSAIDIA KUBEBA CHANGAMOTO [MISALABA] YA MAISHA


Kama Ni Mfuatiliaji Wa Ukurasa Huu, Naamini Utakuwa Unaelewa Kuwa Kila Mtu, Bila Kujali Jinsia Yake, Hali Yake Ya Sasa Ya Kiuchumi Nk, Ni Mfalme Kwa Kuwa Ameumbwa Na Mungu Kwa Sura Na Mfano Wake Na Kupewa Wajibu Wa Kuzaa, Kuongezeka Na Kutawala (Mwanzo 1:26-29).

 Hivyo Wewe Unayesoma Ujumbe Huu Kwakweli Ni Mfalme KWA NAMNA MUNGU AKUONAVYO, Hata Kama Hauna TAJI KICHWANI, FIMBO YA KIFALME MKONONI WA...LA PETE KIDOLENI AU JOHO LA KIFALME MWILINI MWAKO... Hali Yako Ya Nje Haibadili Ukweli Kuwa Mungu Amekuumba UMILKI NA KUTAWALA!


SOMO LA LEO
Wote Tunajua Kuwa BWANA YESU NI MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA WOTE!
Lakini Nabii Isaya Wakati Anatabiri Juu Ya Kuzaliwa Kwa MFALME YESU Miaka Zaidi Ya 600 Kabla Ya Tukio La Kuzaliwa Kwake, Alisema Kuwa Yesu ANAO UWEZO WA KIFALME MABEGANI MWAKE (Isaya 9:7).
Na Wakati Yesu Anakwenda KUSULUBIWA Baada Ya Kuchapwa Mijeledi, Kutemewa Mate Na Kufanyiwa Kila Dhihaka, Bado Pia ALIBEBESHWA MSALABA MABEGANI MWAKE... Na Ni Mabega Hayo Hayo YALIYO NA UWEZO WA KIFALME!

CHA KUJIFUNZA
Kilichomsaidia Yesu KUUHIMILI MSALABA Ulikuwa Ni Ule UWEZO WA KIFALME MABEGANI MWAKE!
Kama Nawe Ni Mfalme, Tunatarajia Uwe Na Uwezo Wa KUBEBA MISALABA YA MAISHA Kwenye 'MABEGA YAKO YENYE UWEZO WA KIFALME'
Kama Una Mpango Wa Kuwa Mfalme Na Kukaa Kwenye Kiti Cha Ufalme, Anza Kujifunza Taratibu Namna Ya Kubeba Misalaba UNAYOBEBESHWA NA WATU Kinyume Chako! Unapoanza Kufanikiwa, Hata Marafiki Watakuwa Adui Zako, Uliwasaidia Watakugeuka Na Kukusema Kwa Mabaya... Kitakachokusaidia Kulinda Nafasi Na Hadhi Yako Kama MFALME Ni Kujua Namna Ya Kutuimia Uwezo Wako Wa Kifalme MABEGANI MWAKO KUBEBEA MISALABA UTAKAYOBEBESHWA!
Kama Yesu Aliweza, Nawe Pia Utaweza... Maana Tunayaweza MAMBO YOTE [Kubeba Misalaba Kukiwemo] Katika Yeye Kristo Yesu Atutiaye Nguvu (Wafilipi 4:13)!

Wewe Ni Mfalme, Endelea Kujifunza Kanuni Za Kifalme Ili Muda Wa Wewe Kuwa Mfalme Ukifika Usisumbuke Katika Kuishi Na Kutenda Kama Mfalme!

Wako,
Mfalme, Mwl Dickson Cornerl Kabigumila

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.