DIAMOND PLATNUMZ AREKODI WIMBO NA JOYOUS CELEBRATION

Diamond akiwa na waimbaji mbalimbali wakiwemo wa Joyous celebration jana asubuhi studio za SABC.

Mwimbaji wa muziki wa nje ya kanisa nchini Nasibu Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz ni mmoja kati ya waimbaji wengine wengi wa Afrika walioshiriki pamoja na kundi maarufu la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini kurekodi wimbo wa pamoja kupiga vita gonjwa la ebola, wimbo ambao ni wazo na utunzi wa Joyous Celebration.

Kazi ya kurekodi video wimbo huo imefanyika katika studio za shirika la utangazaji la Afrika ya kusini SABC nchini Afrika ya kusini huku umoja huo wa wasanii walioimba wimbo huo wakitumia jina la wimbo maarufu ulioimbwa na waimbaji nyota wa nchini Marekani kusaidia Afrika wa 'We are the world wenyewe wakiongeza neno Afrika mbele yake.

Ukiacha kundi la Joyous pia kulikuwa na waimbaji wengine kutoka Afrika ya kusini kama Mahottella Queens, Mafikizolo na wengineo pamoja na waimbaji kutoka Nigeria na pande nyingine za Afrika, Tanzania ikiwa imewakilishwa na mwimbaji huyo ambaye pia alijinyakulia tuzo tatu kati ya nne alizokuwa anawania zilizokuwa zimeandaliwa na kituo maarufu cha Channel O cha nchini humo.

Baadhi ya waimbaji wa Joyous Celebration wakipata picha ya pamoja

Waimbaji wa Joyous wakipata picha ndani ya studio

Sylvester Funani wa Joyous akiwa na waimbaji wa Mahottella Queens.

Picha kwahisani ya Diamond na Sylvester Funani
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.