DKT SLAA MGENI WA HESHIMA KANISANI KWA GWAJIMA JIONI YA LEO


Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo nchini (chadema) Wilbroad Slaa anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima katika ibada maalumu ya kufunga mwaka iliyoandaliwa na kanisa la Ufufuo na Uzima nchini ambalo kwa jijini Dar es salaam hufanyia ibada zao katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe.

Katika taarifa kupitia ukurasa wao wa Facebook kanisa hilo limesema ibada hiyo inatarajiwa kuanza majira ya saa 12 jioni ikifuatiwa na ibada kubwa ya kuukaribisha mwaka mpya. Katika ibada hiyo kutakuwa na kipindi cha maombi kwa watu wenye shida mbalimbali, ambapo kanisa hilo linaingia mwaka mpya wa 2015 kwa neno "Tiisha miliki tawala".
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.