FAMILIA YATOA RUHUSA KWA JOYOUS KUENDELEA NA RATIBA ZAKE, WAIMBAJI WENGINE WAFARIKI DUNIA

Marehemu Lihle wa kwanza kushoto akiwa na rafikize, Ntokozo, Hlengiwe na Kuki 
Kundi la Joyous Celebration linatarajiwa kuendelea na ratiba yake ya uimbaji mwishoni mwa wiki hii baada ya kuambiwa kufanya hivyo na familia ya aliyekuwa mwimbaji wao marehemu Thembelihle Mbanjwa Sowazi aliyefariki kwa ajali ya ajali jumapili asubuhi nchini Afrika ya kusini.

Katika taarifa yake kundi hilo limesema familia ya marehemu imetaka Joyous kuendelea na shughuli zake kama kawaida kama ilivyokuwa imejipangia ratiba yake awali kabla ya kutokea kwa msiba huo kwakufanya hivyo itakuwa njia moja wapo nzuri ya kumuenzi mwimbaji mwenzao kauli ambayo imepokelewa kwa mikono miwili na kundi hilo.

Ambapo kundi hilo limetangaza kwamba kuanzia mwishoni mwa wiki hii maonyesho yao yote wanayatoa katika kumuenzi mwimbaji mwenzao wakianzia nchini Swaziland kisha Kenya na baadaye tarehe 19 na 20 tukio lao la kurekodi DVD ya 19 pia itakuwa maalumu kumuenzi na kumkumbuka Lihle ambaye alikuwa mmoja kati ya waimbaji nyota na wakutegemewa kwa upande wa sauti ya kwanza. Aidha siku ya leo katika makanisa mawaili nchini Afrika ya kusini kutafanyika ibada maalumu ya kumuenzi marehemu Thembelihle Mbanjwa Sowazi huku ibada ya mazishi yake inatarajiwa  kufanyika kesho saa 2 asubuhi katika kanisa la Grace Bible lililopo Pimville Soweto.

Wakati huo huo mwanakaka Siyabulela Sabu Satsha mpiga ngoma (drum) maarufu wa kundi hilo ambaye alikuwa mmoja wapo wa wahanga wa ajali hiyo iliyomuacha katika hali mahututi ya kutojitambua na kulazwa hospitalini, hapo jana asubuhi aliweza kuamka na kuweza kuzungumza na watu waliomtembelea na kutuma salamu zake za shukrani kwa maombi yao.

Siyabulela Sabu Satsha.


Kundi la Joyous kupitia ukurasa wake wa Facebook uliwaomba wapenzi wa kundi hilo kujiunga nao katika kumuombea mpigaji huyo siku ya jumatatu saa moja usiku popote pale walipo, jambo ambalo lilitekelezwa na majibu yameonekana kwa mpigaji huyo kuamka na kuzungumza na wapendwa wake.


Aidha katika taarifa nyingine kutoka nchini Afrika ya kusini waimbaji wengine wawili wa nyimbo za injili wametwaliwa na Bwana, akiwemo mwanadada Lulu Dikana ambaye alikuwa anatarajiwa kufanya onyesho siku ya leo huko Durban, ambapo katika taarifa imeelezwa mwimbaji huyo aliwekwa hospitali kwa uangalizi siku ya jumanne kutokana na kutojisikia vizuri na uhai wake kuishia hapo siku ya jana jumatano. Mwimbaji huyo pia ana dada yake aitwaye Zonke Dikana wote wakiwa wanafanya kazi chini ya mkataba na kampuni ya Universal Music. 

Mwimbaji mwingine ni kijana Fest Igear Enamandla Ntengento ambaye amefariki dunia siku ya jumanne ikiwa siku moja tu aandike kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba hata kama akiondoka leo…angalau amejaribu  

if i leave now....atleast....i tried.
Like ·  · 
                    BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.