JOHN LISU AKATA KIU YA KUKOSEKANA KWA MIAKA 15 MKOANI MBEYA

Siku ya jumapili iliyopita  December 14 katika jiji la Mbeya ilikuwa ni siku ambayo muabudu John Lisu akiwa na timu nzima walimtukuza Mungu pamoja na wakazi wa jiji hilo waliohudhuria katika Uko Hapa Tour The Sound of Worship ndani ya ukumbi  wa St Mary's ambao upo maeneo ya Forest mpya.


Hii ilikuwa ni mara baada ya miaka 15 kupita tangu John Lisu akanyage jiji hilo kihuduma mnamo mwaka 1999 ambapo alienda kuhudumu kwenye mkutano wa injili. Kuonyesha kuwa watu walikuwa na kiu ya kumwabudu Mungu pamoja na John Lisu, walijitokeza kwa wingi kiasi cha kuwashangaza hata wenyeji wa jiji hilo kwani walitegemea watu kuwa wachache kutokana na gharama za kuchangia mlangoni.

Mishale ya saa tisa tamasha lilianza kwa Praise team kutoka T.A.G Forest ya Kwanza kupanda na kuimba wimbo wa kuabudu baada ya hapo Mchungaji Tambikeni kutoka kanisa hilo alifungua kwa maombi. Kisha Mc akachukua nafasi yake kwa kuanza kuwaita waimbaji waliofika kushiriki na Lisu.

Muimbaji aliyeanza ni TUNTUFYE

baada ya hapo PETER MBUMBA

Kisha MWANJISI akachukua nafasi

IMMA MOPAO akamtukuza Mungu kwa solo gitaa

Kijana JOEL nae akafuatia

AMBWENE MWASONGWE akachukua nafasi

Baada ya hapo PRAISE TEAM T.A.G FOREST YA KWANZA

Dr CHACHA akapata nafasi ya kuwashirikisha watu neno la MUNGU

Hatimaye JOHN LISU na TEAM NZIMA wakapanda

Ni baadhi ya picha za Uko Hapa Tour The Sound of Worship jijini Mbeya. Picha zaidi zinakuja muda si mrefu endelea kuwa karibu na Gospel Kitaa.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.