JOHN LISU NA UKO HAPA TOUR MBEYA JUMAPILI HII

Baada ya Uko Hapa Tour kufanyika katika jiji la Mwanza hatimaye Muimbaji John Lisu akiwa na timu nzima kesho Jumapili Disemba 14 atakuwa katika ukumbi wa St. Marry maeneo ya Forest Mpya jijini Mbeya.

Akizungumza na Gospel Kitaa Lisu amesema anamshukuru Mungu kwa kumfikisha salama katika jiji la Mbeya akiwa na timu nzima na kusema kuwa wakazi wa jiji hilo ni vyema wakajitokeza kwa wingi siku ya kesho Jumapili katika ukumbi wa St. Marry kujumuika pamoja katika kumwabudu na kumtukuza Mung.

John lisu ameongeza kuwa kesho muziki utapigwa live huku pia akiwataja waimbaji watakao msindikiza ni pamoja na Ambwene Mwasonge, Emmmanuel Mgogo pamoja na wengine wenge, na kwamba mlangoni kiingilio kitakuwa ni elfu kumi (10000) Viti maalum, elfu tano (5000) kwa viti vya kawaida na watoto wakichangia elfu tatu (3000).

Gospel Kitaa itakuwepo ndani ya jiji la Mbeya, karibu tujumuike pamoja kwa utukufu wa Mungu.Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.