JOYOUS CELEBRATION YAMWITA MUME WA MWIMBAJI WAKE KUOKOA JAHAZI

William Sejake akimsifu Mungu

Mume wa mwimbaji nyota wa zamani wa Joyous Celebration Tebello Sukwene aitwaye Bafana Sukwene ameitwa na kundi hilo ili kuokoa jahazi katika idara ya kupiga ngoma(drum) baada ya mpigaji wao Siyabulela Satsha bado anaendelea na matibabu baada ya ajali mbaya ya gari iliyopelekea mmoja wa waimbaji wa Joyous Lihle Mbanjwa kufariki dunia.

Bafana ambaye hupiga drum na kundi la mchungaji Solly Mahlangu na waimbaji wengine wa nchini humo alikuwa kati ya waimbaji na wanamuziki wa kundi hilo waliosafiri kuelekea nchini Swaziland kwaajili ya onyesho siku ya jumamosi likiwa na mafanikio makubwa kwa mahudhurio ya mashabiki pamoja na huduma njema iliyofanywa na kundi hilo.

Ambapo endapo hali ya Sabu kama haitakuwa imetangemaa, kuna uwezekano kundi hilo likamtumia Bafana ama Irebolaji mpiga drum wao namba mbili waliyempata baada ya usaili mapema mwaka juzi baada ya Sabu kutangaza kuachana na Joyous kisha kundi hilo kumuomba aendelee nao kwa recording ya 18 lakini mpaka sasa bado yupo na kundi hilo.

Bafana Sukwene akiziba pengo la Sabu kwa muda

Aidha ukiachana na Bafana ambaye mkewe Tebello kwasasa anatamba na album yake binafsi iitwayo 'He's Alive' pia katika msafara huo walikuwepo waimbaji wengine nyota waliowahi kutamba na Joyous kabla ya kumaliza mkataba wao akiwemo mwimbaji aliyetokea kupendwa sana na mashabiki wa kundi hilo William Sejake aliyetamba na wimbo O muhao, wengine ni Sbongiseni, Nhlanhla Mwelase pamoja na mwanadada Mercy Ndlovu Manqele ambaye alionekana hata kwenye onyesho la Kimberley huku taarifa zisizo rasmi zikidai mwanadada huyo ameamua kurejea kundini baada ya kuwakilisha vyema nyimbo za kabila lake la Tsonga.

Mercy Ndlovu Manqele akiwakilisha

Wakati huohuo wapenzi wa Joyous nchini Kenya watapata wasaa wa kuliona kundi hilo wiki hii litakapofanya onyesho lake nchini humo. Ambapo tayari baadhi ya wafanyakazi wake wameshawasili nchini humo.

Sbongiseni akimsifu Mungu

The Band

Baadhi ya umati wa mashabiki nchini Swaziland wakienda sambamba na Joyous jumamosi iliyopita.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.