KWA TAARIFA YAKO: BAADHI YA MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU REKODI YA 19 YA JOYOUS

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO ni kwamba leo tupo Afrika ya kusini na tutakujulisha jambo moja kuhusiana na kundi maarufu la muziki wa injili Afrika la Joyous Celebration. Kama ujuavyo kundi hili lilirekodi CD na DVD ya 19 wiki iliyopita katika moja ya kanisa huko kitongoji cha Soweto jijini Johannesburg Afrika ya kusini. 

KWA TAARIFA YAKO tangu kuanzishwa kwa kundi hili miaka takribani 22 iliyopita hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa kundi la Joyous kurekodi DVD yake ndani ya Soweto jambo ambalo lilipokelewa kwa shangwe hasa ukizingatia kundi hilo halina mpinzani nchini kwao kutokana na kukubalika hata kualikwa kwenye matukio makubwa ya kitaifa ikiwemo msiba wa Rais Nelson Mandela, na hata kusafiri hadi nchini Cameroon ambako walialikwa na ubalozi wa Afrika kusini nchini humo kusherehekea sherehe ya taifa lao nchini humo.
KWA TAARIFA YAKO licha ya kwamba kitongoji cha Soweto kilikuwa kikijulikana sana kwa umasikini na hali ya hatari kutokana na vitendo vya wizi lakini pia ndicho kitongoji kimojawapo huwezi kukisahau unapozungumzia uhuru ama ubaguzi uliokuwa nchini humo enzi za ukoloni. Joyous waliamua kurekodi album yao katika kitongoji hicho kwasababu ya kusherehekea kukua kwa demokrasia nchini kwao toka Rais wao hayati Nelson Mandela alipokamata usukani wa kuiongoza nchi hiyo. 

KWA TAARIFA YAKO kwa mara ya kwanza kundi hilo limerekodi na waimbaji watatu kutoka
Zimbabwe katika rekodi yao ya 19 akiwemo mwimbaji maarufu aitwaye Takesure Zamar, Eric Moyo ambaye amewahi kushinda shindano la Idols Afrika pamoja na Mkhululi ambaye bado yupo na Joyous. Kwa kawaida Joyous toka imeanzishwa ina miji maalumu ambayo hufanya rekodi zao lakini siku za karibuni mambo yamebadilika baada ya kuanza kuingia katika kumbi za miji tofauti kwa maonyesho ikiwa pamoja na kuchagua maeneo tofauti ya kufanya rekodi xao kwasasa.


Angalia wimbo mpya utakaokuwemo kwenye DVD mpya uitwao Kuregerera In advance ulioimbwa na Zamar kama ulivyorushwa na SABC1 siku ya jumapili mara baada ya rekodi ya kawaida kuisha jumamosi. Nyimbo zilizorushwa inadaiwa kundi hilo lilibadili baadhi ya vipande ili kutofautisha na jinsi walivyorekodi ijumaa na jumamosi.


Eric Moyo akiimba kwahisia
KWA TAARIFA YAKO asilimia kubwa ya waimbaji waliopo na waliomaliza mkataba wao na Joyous wanatokea Durban nchini humo jambo ambalo hutajwa kama Joyous makao makuu yake ni Durban na ni lazima kila mwaka inapofanya tour zake lazima ifanye onyesho la siku mbili Durban kutokana na kuwa na mashabiki wengi na tiketi zao huisha mapema kabla ya maonyesho. KWA TAARIFA YAKO kutokana na mpiga ngoma wake Siyabulela Satsha kuwa mgonjwa, kundi hilo halikuweza hata kumtumia mpiga ngoma wao namba mbili aitwaye Irebolaji waliyempata baada ya Sabu kutangaza kumaliza na Joyous badala yake kundi hilo likaamua kumtumia Bafana Sukwene mume wa mwimbaji wake wa zamani Tebello Sukwene aliyemaliza mkataba wake.
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo….

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.