MCHUNGAJI NA FAMILIA YAKE TOKA AFRIKA YA KUSINI WAUWAWA NA TALIBANI AFGHANISTANI

Nyumba ikiteketea kwa moto baada ya shambulio hilo©Reuters/Omar Sobhani
Mchungaji Werner Gronwald raia wa Afrika ya kusini ameuwawa na wapiganaji wa taleban pamoja na watoto wake wawili nchini Afghanistan akihofiwa kuwa ni mmishenari aliyekwenda nchini humo kwa kificho ili kufundisha habari za Kristo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Christian Post umeandika kwamba wapiganaji wa kundi la Talebani walishambulia nyumba aishiyo mchungaji Gronwald (46)na familia yake mara tatu kwa muda wa masaa matatu kabla ya mlipuko mkubwa ulioangamiza familia hiyo huku mke wa mchungaji huyo Hannelie akisalimika kwakuwa alikuwa kazini wakati tukio hilo linatukia.

Mchungaji Gronwald alikuwa akifanya kazi kwa kushirikiana na shirika la maendeleo ya elimu (Partnership in Academics and Development PAD) la Marekani ambalo lilianzisha huduma zake nchini Afghanistan kwa miaka 12 sasa. Mchungaji huyo aliuwawa wiki iliyopita pamoja na watoto wake wawili wa kiume na wa kike wenye umri wa miaka 17 na 15 jijini Kabul katika nyumba za PAD walikokuwa wakiishi.

Kwa mujibu wa dada wa Hannelie amesema mdogo wake amepoteza karibu kila kitu akiwemo mumewe na watoto wake. "Kila kitu kimeteketea, Hannelie alikwenda nyumbani na hakukuwa na chochote, bado yupo Kabul na sasa tunajaribu kutafuta njia ya kumrudisha nyumbani pamoja na miili ya familia yake" alikaririwa Riana du Plessis dada wa Hannelie akiongoa na local news outlet.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.