NYOTA WA MUZIKI WA INJILI MAREKANI NA FAMILIA YAKE WAANDAMANA

Nyota wa muziki wa injili duniani Donnie McClurkin alikuwa mmoja kati ya maelfu ya wakazi wa jiji la New York nchini Marekani ambao waliandamana katika kampeni inayoendelea ya kupinga kuuwawa kwa wanaume weusi wasiokuwa na silaha kunakofanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo.

Katika maandamano hayo McClurkin aliandamana pamoja na dada yake mchungaji Andrea Mellini McClurkin aliyeambatana na mumewe Louis Mellini pamoja na watu wa karibu wa mwimbaji huyo pamoja na waimbaji wengine na watu maarufu ambao tokea kutokea kwa kifo cha bwana Eric Garner wa Missouri aliyefariki wakati akikamatwa na polisi akilalamika kwamba hawezi kupumua hali iliyomfanya kufariki dunia.

Kampeni hiyo ambayo inaendelea kuchukua sura katika miji mbalimbali nchini Marekani imekuja kufuatia kufutwa kwa kesi za askari wote waliohusika na mauaji ya watu hao. Ambapo katika maandamano hayo watu wote hutumia neno 'Siwezi kupumua' ama 'I can't Breath' ikiwa neno alilosema marehemu Garner.

Mamilioni wakiwa wamekusanyika jijini New York kupinga mauaji.
Mchungaji Donnie McClurkin akiwa na shemeji yake Louis Mellini katika maandamano hayo

Dada yake Donnie, mchungaji Andrea Mellini akiwa na mumewe katika maandamano hayo
Kitu kimoja kutetea usawa
Baadhi ya umati wa watu waliokuwa katika maandamano hayo
Louis akichukua picha ya pamoja ©Perfecting Faith Church 


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.