RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA ATEUA MMOJA MPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete©Wavuti

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mkuu Mpya mmoja wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi wengine sita kuanzia juzi, Jumamosi, Desemba 6, 2014.

Taarifa iliyotolewa jana, Jumapili, Desemba 7, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Ndugu Ntibenda ataapishwa leo, Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar Es Salaam.

Taarifa hiyo inasema kuwa wakuu waliohamishwa vituo vya kazi ni Mheshimiwa Elaston Mbwilo anayehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda Mkoa wa Simiyu ambako anachukua nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa, Mheshimiwa Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa wa Manyara kutoka Mkoa wa Morogoro na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa Morogoro kutoka Mkoa wa Tanga.

Wengine ni Mheshimiwa Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa Mkoa wa Tanga kutoka Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa Mhandisi Evarist B. Ndiliko anayehamishiwa Mkoa wa Pwani kutoka Mkoa wa Arusha.


Wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu Dar es Salaam.

6 Desemba,2014

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.