SHINDANO LA NINAWEZA KUIMBA UPOKEAJI SAUTI KUFUNGWA USIKU WA LEO


Hatimaye zoezi la upokeaji sauti katika shindano la kusaka vipaji vya uimbaji la Ninaweza Kuimba linatarajiwa kufungwa rasmi leo jumatano majira ya saa 5:55 (23:55) usiku kwa saa za Afrika mashariki. Ambapo mpaka sasa watu mbalimbali wakazi wa mikoa husika kwa shindano hili kwa awamu ya kwanza Arusha na Dar es salaam wametuma sauti zao ambazo zinadhihirisha watu kuwa na uwezo wa uimbaji. Kwawewe ambaye hujatuma sauti yako fanya hivyo kabla ya saa 5:55 usiku ili usipoteze fursa hii muhimu ya maisha yako na huduma kwa ujumla.

Ninaweza kuimba imezinduliwa ili kuwapa nafasi wale wanaoweza kuimba lakini hawakupata fursa ya kuingia studio, kuwezeshwa kurekodi album pamoja na video. Yaani mshindi wa kwanza kupelekwa studio kwa ajili ya kurekodi album yenye nyimbo nane pampja na video zake, na pia washindi wengine wanne kurekodi album ya pamoja na video (kila mmoja nyimbo mbili mbili).

Shindano hili ambalo limezinduliwa mwezi Novemba, linaratibiwa na kampuni ya Tuck & Roll,
kampuni mama ya Gospel Kitaa na InHouse, pamoja na wadau wengine kama vile JM Media, Araka Pro Media, na wengineo wengi ambao bado wako kwenye hatua za mwisho za makubaliano ili kujua namna ya kuwezesha washindi.

Ufafanuzi:
Baadhi ya washiriki ama watarajiwa washiriki wamekuwa na maswali namna ya kushiriki, Maelezo ya jumla yanapatikana (bofya hapa) lakini kwa ajili ya ufafanuzi kwa wale wote ambao wanapenda kushiriki (Arusha na Dar es Salaam) yafuatayo ni maelekezo;

NAMNA YA KUTUMA:
Tumia simu yako kurekodi sauti yako ukiimba wimbo ubeti mmoja (wowote) na kiitikio cha wimbo wa Ni Tabibu wa Karibu, na kisha uitume kwa njia ya WhatsApp na kisha uitume kwenda namba moja tu kati ya 0769952893 ama 0713554153. Mara baada ya kutuma, utapata ujumbe kuthibitisha sauti yako kupokelewa.

Kama unatuma sauti yako kwa njia ya mtandao tofauti na WhatsApp, basi unaweza kufanya hivyo kwa kuituma kwa barua pepe kwenda uimbaji@inhouse.co.tz Halikadhalika pia utafahamishwa sauti yako itakapotufikia. Iwapo kuna mapungufu kwenye taarifa zako, basi utafahamishwa. Mfano umewekwa.

Iwapo ndani ya masaa 24 tokea utume sauti yako haukupata mrejesho, basi unaweza kuituma tena kwa mfumo uleule kama wa awali. Kama ni kwa barua pepe basi ufanye vivyo hivyo, halikadhalika kwa WhatsApp.

Kila la heri kwa washiriki wote.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.