SOMO: HAKUNA MFALME KWA KUZALIWA TU KWENYE UKOO

©Precision Graphics
HAKUNA MFALME KWA KUZALIWA TU KWENYE UKOO/ FAMILIA YA KIFALME; LAZIMA UPITE SHULE YA UONGOZI NA UTAWALA ILI KUIWEKA AKILI NA FIKRA ZAKO SAWA!

Mungu Alimtuma Nabii Samweli Aende Kwenye Nyumba Ya Mzee Yese Ampake Daudi Mafuta Ili Awe Mfalme Mahali Pa Mfalme Sauli (1 Samweli 16). Lakini Bado Ilimchukua DAUDI Miaka Mingine Zaidi Ya 13 Kuja KUKAA KWENYE KITI CHA KIFALME... Alitazamwa Na Mungu Kama Mfalme Akiwa Na Miaka 16 Kuelekea 17 Lakini Alikuja KUPATA UHALISI WA KUWA MFALME Akiwa Na Miaka 30!


NI KWANINI MUNGU HAKUMPELEKA IKULU MOJA KWA MOJA MARA BAADA YA KUMPAKA MAFUTA?

Jibu Ni Rahisi; KUMCHUKUA MCHUNGA KONDOO PORINI KULE MACHUNGANI NA KUMLETA IKULU AWE MFALME, BILA KUMPA SHULE YA UONGOZI, UTAWALA, USIMAMIZI NA UZOEFU WA WATU NA MAISHA, YALIKUWA MAJANGA... SAWA NA KUMPA KICHAA RUNGU!

Ndio Maana Mungu Alitumia Miaka Zaidi Ya 13 Akimwandaa Daudi KUKAA KATIKA KITI CHA UFALME; JAPO TAYARI ALIKUWA MFALME KWA KULE KUPAKWA MAFUTA!

SIRI YA KIFALME; Hata Wewe Mungu Amekuweka Kuwa Mfalme, Amekupa SURA NA MFANO WAKE, AMEKUBARIKI ILI UWE NA UWEZO WA KUZAA NA KUONGEZEKA... Lakini Bado Hawezi KUKUKABIDHI KITI CHAKO CHA UFALME MPAKA PALE ATAKAPOHAKIKISHA UMEFUZU MADARASA ANAYOKUPITISHA SASA KATIKA MAISHA!
Usiwe Na Haraka, Usikate Tamaa, Weka Bidii Kumjua Mungu Zaidi, Baada Ya Muda UTAFUZU NA UFALME WAKO UTAKABIDHIWA NA UTAMILKI NA KUTAWALA!
Uwe Na Subira, Uwe Na Uvumilivu, Usikubali Kuchoka Njiani... Wewe Ni Mfalme, Hakikisha UMEFIKIA MAHALI PAKO PA MAMLAKA, Hakikisha UMEKALIA KITI CHAKO CHA ENZI!

Mfalme Ninakusalimia,
Mfalme, Mwl D.C.K

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.