SOMO: MUNGU WA DUNIA HII - MCHUNGAJI GWAJIMA

Mchungaji Josephat Gwajima


 Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. 2Wakorintho4

Shetani ana majina mengi na mojawapo ni mungu wa dunia hii.

Nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao. Kutoka6: 3

Mungu alimtokea Musa akamwambia “mimi ni Mungu mwenyezi” maana yake ni Mungu wa juu sana, ni Yehova, ni Mungu wa Ibrahim. mungu wa dunia hii ana jina jingine anaitwa mkuu wa ulimwengu na huyo sio Mungu wetu sisi. Mungu wetu sisi ni Mungu wa mbingu na nchi ambaye wana wa Israeli wanamwita Yehova, mahali anataka kujionyesha nguvu zake anaitwa “Jehoiva eljido”, Jehova nisi maana yake“bendera yenu”, Jehova rohi “Bwana mchungaji wangu”.

Kwenye agano jipya aliamua kuvaa mwili akazaliwa na tukauona utukufu wake. Alikuja kwa njia ya neno na kupitia neno hilo akazaliwa akavaa mwili akaitwa Yesu. Kwenye agano la kale utaona imeandikwa “kisha neno la Bwana likamjia Yeremia na kusema hili neno la Bwana ni Mungu”.

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza. Yohana1:1
Yesu kristo maana yake nyingine ni Yehova amashira “Mungu yule yule” duniani hapa kuna mabishano makubwa kuhusu Yesu kuwa ni Mungu lakini ukisema Yesu ni nabii hakuna anaye ongea, ukisema Yesu ni mtume wa myaazi mungu hakuna anaye bisha lakini ukisema kuwa Yesu kristo ni Mungu panatokea kutoelewana na dunia inatikisika.
Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. Yohana12:31
Mungu wa dunia hii anaitwa mkuu wa ulimwengu
Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu. Yohana14:30
Kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa. Yohana 16:11
Mungu wa dunia hii Yesu kristo naye alimwita mkuu wa ulimwengu, jina jingine anaitwa mwovu maana yake ni mbaya ana uovu ndani yake. Unatakiwa ufike mahali uone sio kila mtu anayesema Mungu atatusaidia anamaanisha Yesu kristo Mungu wa mbingu na nchi wengine wanamaanisha mungu wa dunia hii.
Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. 1Yohana4:4
Ndio maana ya lile andiko linasema ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao, kumbe ndani yetu tuliompokea Yesu kwenye mioyo yetu kuna Mungu wa Mbingu na nchi lakini ndani yao kuna mungu wa dunia hii ukiwaambia mtu anaweza kufa na kufichwa shimoni, wanakataa, ukiwaambia mtu anaweza kufufuka hawakuelewi! Ni kwasababu ndani yao kuna mungu wa dunia hii amekaa na kupofusha fikra zao.

Kuna nguzo NNE zinazoiendesha dunia
1. Siasa
2. Uchumi
3. Dini
4. Jeshi
Sehemu hizi mungu wa dunia hii amezikamata na kuziendesha na unapotaka kuingia kwenye sehemu ya siasa lazima uchafuliwe kwanza kwa wizi na mambo mengine ndipo utawale kwenye siasa. Lakini Mungu akaaye ndani yetu atazuka katika uso wa nchi na kuziangusha tawala zote za ufalme wa mungu wa dunia hii kwa jina la Yesu.
Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu. Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele. Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. 1Yohana5:19
Andiko hili linamaanisha dunia yote inaongozwa na yule mwovu ambaye ni mkuu wa ulimwengu au mungu wa ulimwengu. Watu wa dunia hii kwenye zile nguzo nne kwa kadri mtu anavyo ongezeka kwenye uchumi, siasa ndivyo anazidi kuwa mbaya zaidi kwasababu amepofushwa fikra zao na wanaona ni kawaida kwa mambo mabaya wanayo yafanya kumbe mungu wa dunia hii ndiye anaye waongoza.
Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa. Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu. Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana. 1Wakorinto1:20
Kuna watu wengine wana hekima ya dunia wanaweza kuongea maneno ukadhani ni Mungu wa mbingu na nchi anaongea kupitia yeye kumbe ni mkuu wa ulimwengu/mungu wa dunia hii. Kuna watu wanatumia hekima ya dunia hii kutawala dunia, kumiliki na kufanya bihashara.

Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu; lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. 1Wakorinto2:6-
Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani. Yakobo3:15
“Kitu cha kidunia ndicho hicho hicho cha kibinadamu na ndicho hicho hicho cha kishetani”. Tunaungana na watu ili kuwabadilisha wao wawe sehemu yetu na sio kuwa sehemu yao na ni vuzuri unapokwenda sehemu yeyote uwe makini wasikubadilishe kuwa sehemu yao. mungu wa sistimu za siasa, fedha, dini ni mungu wa uongo na kupofusha fikra za watu.
Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Luka4:1-5

Shetani alimpandisha Yesu na kumwonyesha miliki za dunia na fahari kwa dakika moja akamwambia mimi (ibilisi) humpa yeyote nipendavyo ila akiniabudu, kumbe kila aliye kwenye nguzo za dunia amepata kwa Bwana wa majeshi, ama kwa ibilisi mkuu wa dunia hii, Shetani aliuchukua utawala wa dunia hii kutoka kwa Adamu na kuigeuza kuwa kama ilivyo hata Adamu akija ataona jinsi dunia ilvyo tofauti na alivyoiacha kwasababu ya uharibifu wa mungu wa dunia hii.

Ulimwengu uko chini ya yule mwovu mungu wa dunia hii asiye waacha wafungwa wake waende zao.

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Warumi 12:2

Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele. Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake. Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, mwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake. Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye. 1yohana2:15
Dunia na tama yake vinapita bali yeye alishikaye neno lake adumu milele. Mungu anaye tupenda ametuweka kwenye dunia ambayo mkuu wake ni ibilisi na ndio maana Yesu alipoanza kuwafundisha watu jinsi ya kuomba alisema ‘Baba yetu uliye mbinguni’ maana yake sio marekani na ‘jina lako litukuzwe’ maana yake sio dogo ufalme wako uje maana yake kabla Yesu hajanyakua kanisa ufalme wake utakuja.

Mungu alimwacha shetani ajenge tawala wake hapa duniani ili amtume Yesu kama nuru auokoe ulimwengu. Ndio maana imeandikwa “na ile nuru ya ngaa gizani nalo giza halikuweza kuishinda” kwa sababu hiyo Yesu kristo alidhihirishwa ili kuudhihirisha uweza wake. Ndio maana Yesu alipomtokea Yohana kwenye kisiwa cha patimo alimwambia ayaandike mambo yaliyopo na yatakayokuja

Kazi yetu ni kuwapunguza waingiao motoni na kuwapeleka mbinguni. Na watakao kwenda mbinguni ni wengi kuliko watakao kwenda motoni.

Mungu wa dunia hii ndio anaitwa lucifa, baba wa uongo, ibilisi, mfalme wa giza, lakini ni Mungu na mtu anaweza kusema nampenda mungu chunguza anaweza kuwa mungu wa dunia hii “shetani”

Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao. Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. Yohana17:9
Anajua ulimwengu unashetani ambaye ni mkuu wake hivyo hawezi kuuombea na ulimwengu umewachukia kwakuwa sio wa ulimwengu huu ndio maana watu wanaweza kukuchukia ni kwasababu wewe sio wa ulimwengu huu, na Wewe sio wa ulimwengu kama vile Yesu alivyo sio wa ulimwengu alimaliza kazi yake akaenda zake na wewe una kazi hapa duniani zaidi ya kazi unayofanya na unatakiwa uifanye kwa utakatifu ili baadaye urudi mbinguni. Tumetumwa duniani tumepewa kazi ya kufanya hapa duniani lakini mkuu wa giza amekushika kwenye ulevi, ukahaba, wizi, na uharibifu wote lakini umetumwa kutoka mbinguni. Watu wote wametoka mbinguni tatizo hatukumbuki siku tuliyotoka na nini kilichutuleta hapa duniani, baba na mama hutengeneza mwili na Mungu wa Mbingu na nchi huweka roho ndani yake yenye kusudi la kufanya hapa duniani. Binadamu ni roho iliyo ndani ya nyumba inayoitwa mwili na baba wa Roho zetu ni Mungu wa mbingu na nchi ndio maana Yesu alitufundisha jinsi ya kuomba tuombe” Baba yetu wa mbinguni…”
Shetani anachokifanya kwasababu ni mkuu wa ulimwengu huu anajua leo wangapi wamezaliwa na kazi wanayotakiwa kuifanya anachokifanya anawaumiza watu unakuta mtu tangu amezaliwa ni mgonjwa amehangaika hajapata matibabu bado lakini haujachelewa bado unaweza kuamka na kusonga kwenye kusudi lako kwa damu ya Yesu kristo.

“Mungu wa dunia anaweka magonjwa, Mungu wa mbingu na nchi anaweka uzima ndani ya watu kuna vitu elimu ya dunia haiwezi kuyafanya”

Kwa jina la Yesu kristo mkono wa mungu wa ulimwengu huu ulio nyooshwa kwenye maisha yangu nina uvunja kwa jina la Yesu, leo nina rudi kwenye maisha yangu kwa jina la Yesu”
UKIRI
“Inawezekana mkuu wa ulimwengu alikuwekea ugonjwa na anajua bila ugonjwa huo unaweza kumtumikia Mungu wa Mbingu na nchi kwa uaminifu”
Kwa damu ya Yesu ninaziangusha nguzo za mkuu wa ulimwengu kwa jina la Yesu, wale wote mliokaa kwenye nguzo za kisiasa, dini, jeshi na uchumi chini ya mkuu wa ulimwengu ninawaangusha wote kwa jina la Yesu, ewe mkuu wa ulimwengu nakufunga leo kwa jina la Yesu, ninaangusha fikra zako ulizoziweka kwenye maisha yangu kwa jina la Yesu kristo, kila hekima ya mkuu wa ulimwengu ninaiharibu kwa jina la Yesu, kwa mamlaka ya Jina la Yesu kristo ninazikamata nguzo zote za mkuu wa ulimwengu kwa jina la Yesu, ninafuta kila upofu wa mkuu wa ulimwengu kwenye macho yangu, akili yangu, moyo wangu kwa damu ya mwana kondoo katika jina la Yesu, nakunyanganya kazi yangu, afya yangu uliyoigusa kwa mkono wako ewe mkuu wa ulimwengu kwa jina la Yesu kristo. Amen

Inawezekana mtu una matatizo kwasababu shetani amekuwekea matatizo kwasababu anajua utakuwa nani baadaye anajua Mungu wa mbingu na nchi ameweka kipawa cha aina gani ndani yako, mkuu wa dunia hii ndiye anakuzuia ili usije fikia pale unapotakiwa kufika. Shetani hapambani na wewe kwasababu ulivyo anapambana na wewe kwasababu ya kitu ambacho Mungu ameweka ndani yako,

Elimu inatusaidia kuendeleza kile kilichowekwa na Mungu ndani yetu.

“Imeandikwa kabla haujatungwa katika tumbo la mama yako nalikujua” wachawi wanahitaji kile ulichonacho ndani yako ili wakichukue na kuendeleza ufalme wa mkuu wa ulimwengu kwenye siasa, uchumi, jeshi, dini”.

Mashetani, majini, mapepo, mizimu, wagang, wasoma nyota na wengine wote ni watumishi wa mkuu wa ulimwengu.

Ninaamuru nyota yangu ya safari, Kupendwa, Kuhubiri, Biashara inayotumiwa na watu wa dunia hii ninaamuru njooo kwa jina la Yesu kristo Amen.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.