TUJITOKEZE KUPIGA KURA JUMAPILI TAREHE 14 DESEMBA 2014


Siku ya kesho Jumapili tarehe 14 Disemba 2014 ni siku muhimu kwa Tanzania, ambapo wananchi wenye sifa stahiki watajitokeza kupiga kura ya kuchagua viongozi wa Serikali za Vijiji na Mitaa, pamoja na wajumbe.

Hitimisho la kampeni ambalo ni leo, limehitimishwa kwa mbwembwe na wagombea wa kila chama kinachowania nafasi husika, ambapo kwa baadhi ya maeneo shamrashamra zinaonekana dhahiri, huku maeneo mengine yakizidiwa na makelele yasiyo na mpangili (huku harusi, huku sera zikimwagwa)

Cha umuhimu kutoka GK ni kukukumbusha kwamba ni muhimu kujitokeza kuchagua viongozi ambao watawezesha kuifikisha Tanzania kwenye safari yake ya maendeleo, miaka 53 baada ya uhuru wa Tanganyika.

Sikiliza ujumbe kutoka kwa Dr Levy, ambaye anatuasa kuacha fikra potofu kwamba haki iko Mbinguni. Kura yako ndio yenye hatma kuu; Na kwamba hatutakiwi kuigeuza kura mtaji wa biashara. (kwa wenye simu bofa hapa)

Usikose kufika kituo cha kupigia kura kuanzia saa mbili asubuhi, ambapo vituo vitafungwa saa kumi jioni.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.