ULAINI WA KITU HAINA MAANA YA URAHISI WAKE

Na Faraja Naftal Mndeme
GK Contributor
©Jazz Advice
Mara nyingi tumekuwa na hulka ya kurahisisha vitu kuliko ulivyo uhalisia wa vitu kwenye shughuli zetu za kila siku.Mara nyingi tumedharua vitu sababu hatujui gharama ya vitu hivyo kwenye maisha ya watu wengine na uhalisi wa shughuli hizo wanazozifanya. Sisi tunakuja kuona matokeo ya mchakato mkubwa sana ambao wamekuwa nao kwenye maisha yao na kazi zao za kila siku. Mfano "Ni Rahisi kumuona Konda anakusanya nauli kwenye Daladala ukamjibu/kumwangalia kwa kumdharau lakini hujui mpaka ameamua kufikia hapo amepitia nini pia hatujui gharama halisi ya kufanya kazi hiyo sisi tunaona matokeo tu ya kukusanya fedha muda huo, Kama ni rahisi basi jaribu kuifanya wewe utaelewa. "Ulaini wa Kitu Maana yake Sio Rahisi wa Kitu"

Ni rahisi kumuona mwingine amekosea kulio wewe kujiona umekosea.Watanzania tulio wengi tuna kipaji cha kukosoa kuliko kurekebisha kwenye kile mtu anachokosea.Mara nyingi huwa tunaona matokeo tu ya kile mtu anachokianya ndio maana tunapenda kukosoa Mfano"Ni Rahisi kumkosoa mchezaji wa mpira kuwa amekosea angepiga vile angefunga"Lakini tunasahau Gharama ya mazoezi anayoyafanya kufikia pale ni kubwa.Ulaini wa Kitu Maana yake Sio Urahisi wa Kitu.

Mara nyingi tukuwa wavivu kufikiria mara nyingi,Hatupendi kufwatilia vitu ndio maana tunakuwa wepesi wa kuchukukia vitu vyote kuwa ni rahisi sana kumbe sivyo vilivyo kwenye uhalisia."Mfano...Makampuni ya simu yanapotoa matangazo yao wanakwambia hudumu fulani ni Bure,Je kweli ni Bure? Je kwanini Baada ya kumaliza kutangaza utasikia "VIGEZO NA MASHARTI VITAZINGATIWA" Je hivi vigezo na masharti kuzingatiwa ni vipi? Basi kwa maana nyingine kuna gharama ya kulipa inaweza isiwe pesa lakini inaweza kuwa gharama ya kufwata vigezo na masharti inaweza kuwa kubwa zaidi.

Wakati Steve Jobs anaanza kumpuni yake ya kwanza Apple akiwa gereji kwao na Mzee Paul Jobs ilikuwa ni rahisi sana kuwadharau kwa sababu hawakuweza kufikiria mafanikio ambayo leo wangekuwa nayo. Watu wengi leo tunapenda kufurahia mafanikio ya wengine kitu ambacho si kibaya lakini hapo hapo tunayakosoa kwa kusema ningekuwa mimi ningefanya hivi na vile. Ni bora ukae kimiya sababu hakuna mtu anayependa kukosea kwenye maisha kila mtu anapenda kufunya vizuri katika kila kona ya maisha pia kumbuka picha ya ndoto ya mtu anayo mtu mwenyewe na sio mwingine. Gharama ya mtu alolipa mtu mpaka tunafika kuona mafanikio sio ndogo. Leo tuna'touch' tu Ipad na tunafurahia Simu za Iphones lakini haukumbuki kuna mtu alilipa gharama.

Ni vizuri kuwa na mtazamo halisi na gharama halisi na kile unachotaka kukifanya lakini pia ni muhimu kujua vya wengine na gharama za vile vitu wanavyofanya kuliko kukurupuka na kuanza kufikiria katika namna tofauti na jinsi uhalisia wa vitu ulivyo.Penda kufwatilia vitu vizuri kwanza ndipo ufikie kufikia kuhitimisha huku ukiwa na uhakika wa kile unachotaka kukifanya

E-mail:naki1419@gmail.com
+255719742559
God Bless Y’All


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.