VITU VICHACHE VINAVYOWEZA KUONGEZA THAMANI KWENYE MAISHA YAKO YA KILA SIKU

Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.
©Living for a Change
1. JIFUNZE KUWA NA UDHIBITI WA HASIRA ZA HAPA NA PALE
Mara nyingi pale tunapoona vitu havikwenda sawa na vile tunavyotarajia huwa tunapandwa na hasira au jazba.Si mara zote hasira au jazba zinakuwana maamuzi sahihi.Muda mwingi tumeharibu mambo mbali mbali na kushindwa kusonga mbele sababu ya hasira ambazo hazina maana kwenye jambo husika.Mara nyingi tunapopandwa na hasira tunashindwa kufanya maamuzi sahihi sababu kwa muda husika hisia huwa juu,hii inapelekea kufanya maamuzi mengi ukiwa kwenye hisia ambapo ni jambo hatari.Unashauri usifanye maamuzi yeyote pingi unapokuwa na hasira au pindi unapokuwa na furaha iliyopitiliza sababu unaweza kufanya maamuzi yasiyokuwa na tija kwenye maisha yako binafsi na jamii inayokuzunguka pia.

2. JIFUNZE KUDHIBITI MSONGO WA MAWAZO
Hakuna mtu ambaye hakutani na changamoto za kila siku kwenye maisha kwenye mambo mbali mbali yanayotuzunguka lakini cha kushangaza unaweza kukuta wengine wanaweza kuvuka kwa usalama pindi wanapokuwa wamezungukwa na wingi wa misongo ya mawazo.Ni muhimu kuchukua muda wewe binafsi na kujifunza kudhibiti misongo ya mawazo,Maana unapokuwa na misongo ya mawazo mara kwa mara na iliyozidi inapelekea kupunguza utendaji wako wa kila siku kwenye mambo kadha wa kadha lakini pia inaweza kukupelekea kupoteza uhai wako.Tumeshudia watu kadha wakadha wakipoteza uhai wao sababu ya misongo ya mawazo iliyozidi mara kwa mara.Kuongeza ufanisi wako jifunze kudhibiti misongo ya mawazo kwa kuitafutia suluhisho la kudumu na kwa utaratibu usiokuwa na papara wala haraka isiyokuwa na maana.

3. JIFUNZE KUISHI KWA KUWA NA MTAZAMO CHANYA MARA KWA MARA
Muda mwingine tumeshindwa kufanya vyema juu ya mambo mbali mbali sababu ya mitazamo tuliokuwa nayo juu ya maswala mbali mbali.Kama ilivyokujifunza kufanya jambo lingine pia unaweza kujifunza kuwa na mtazamo chanya kwenye mambo mabli mbali hata pale panapoonekana mambo hayendi sawa na taraja lako.Unapokuwa na mtazamo chanya unajitengenezea nafasi nzuri zaidi ya kuweza kufikiria zaidi na kupata suluhisho husika kwenye jambo linalokukabili wakati husika.Muda mwingine sio kama maswali tulionayo yanahitaji majibu makubwa ,muda mwingine yanahitaji kubadili mitazamo mibaya tuliokuwa nayo maishani mwetu kwenye maisha yetu ya kila siku.

4. JIFUNZE KUFANYA MAAMUZI BORA NA MUHIMU
Hakuna mtu alizealiwa akajikuta anaweza kufanya maamuzi bora na kwa usahihi kwenye maisha ya kila siku ,wote tunajifunza kutoka maeneo mbali mbali yanayotuzunga.Ni muhimu kufwata kanuni za msingi za kufanya maamuzi mbali mbali kwenye maisha kuepuka kufanya makosa ambayo yanaweza kukufanya upatwe na hasira au pia ukapatwa na misongo ya mawazo isiyokuwa na ulizama ambayo ungeidhibiti tangu mwanzo.Hakikisha haufanyi haraka haraka kufanya maamuzi muhimu ambayo unajua ukikosea yanaweza kukuletea matatizo mbali mbali.Hakikisha unakuwa na mtazamo zaidi ya mmoja juu ya maamuzi unayotaka kuyafanya kiasi kwamba mtazamo wa kwanza usipofanikiwa ,utaweza kuhamia kwa haraka na upesi kwenye mtazamo mwingine bila kupoteza muda na utakuletea matokeo bora uliyokuwa unayatarajia tangu mwanzo.

5. JIFUNZE KUWA NA MTAZAMO CHANYA KWA WENGINE PIA
Ni rahisi wewe binafsi kuwa na mtazamo chanya kwako binafsi lakini ikawa ngumu kuwa na mtazamo chanya kwa wengine.Ni muhimu usiwe mwepesi wa kuwakosoa kusoa wengine kwa kila wanachofanya,iwapo unaona hawako sawa tumia muda wako kuwarekebisha kwa maana nyingine wape suluhisho badala ya kuishia kukosoa na ukawaacha tu hapo hapo kwa wakati husika.Ni Bora ukakaaa kimiya unapoona hauna suluhisho bora juu ya tatizo la mtu mwingine kuliko uanze kukosoa huku ukijua hauna msaada juu ya tatizo linalomzunguka mwingine.Hakikisha haujengi hisia na mitazamo hasi hata pale watu wanapotofautia na mtazamo wako juu ya maswala mbali mbali kwenye maisha.Jifunzi kuwachukulia katika matazamo chanya kama vile ambavyo wewe ungependa wengine wakutazamo katika mtazamo chanya.

E-mail:naki1419@gmail.com
+255719742559
God Bless Y’All

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.