ASIMAMISHWA KAZI AKIDAIWA KUTAKA KUMBADILI DINI MUUGUZI MWENZAKEMuuguzi aliyefahamika kwa jina la Victoria Wasteney (37) ambaye ni muumini wa dini ya Kikristo amejikuta akisimamishwa kazi baada ya muuguzi mwenzake aitwaye Enya Nawaz kulalamika kwa uongozi kwamba muuguzi mwenzake anataka kumbadilisha dini na kuwa Mkristo.

Kwa mujibu wa Wasteney kama alivyokaririwa na gazeti la Daily Mail la nchini Uingereza amesema taasisi ya huduma ya Afya nchini humo NHS imemfanya aonekane kama mpumbavu wa mambo ya dini baada ya kufanya maombi na muuguzi mwenzake ambaye ni muislamu.

Victoria amesema alisimamishwa kazi akituhumiwa kumdhalilisha na kumkashifu muuguzi mwenzake mara baada ya mwenzake huyo kuuambia uongozi kwamba Victoria anataka kunbadili dini na kuwa Mkristo, hali iliyomfanya muuguzi huyo kufungua mashitaka dhidi ya taasisi hiyo kwakumsimamisha kwasababu ya mambo ya kidini.

Wasteney alikuwa akifanya kazi chini ya NHS katika kituo cha John Howard Centre kilichopo mashariki mwa jiji la London na kwamba Nawaz alijiunga katika hospitali hiyo mwaka 2012 na kwamba kwa pamoja wamewahi kuwa na majadiliano juu ya uislamu na Ukristo ambayo ndiyo yaliyosababishwa kusimamishwa wakati aliyeanzisha mazungumzo hayo alikuwa Nawaz. Victoria amesema Nawaz alimfuata akiwa analia juu ya tatizo lake la kiafya hali iliyomsababisha Wasteney kumuuliza mwenzae kama yupo tayari amuombee jambo ambalo Nawaz alilikubari na kuombewa kisha Victoria alimpa kitabu kuhusu mwanamke aliyebadili dini kutoka uislamu na kuwa Mkristo.

Nawaz aliamua kutoa malalamiko yaliyosababisha Wasteney kusimamishwa kazi kwa miezi nane ili kupisha uchunguzi wa jambo hilo pamoja na barua ya onyo huku akihamishiwa kazi sehemu nyingine. "mimi si pingi uislamu, kila siku niko makini linapokuja suala la imani za watu wengine, tulizungumza kuhusu imani zetu, lakini sikumwambia kwamba imani yangu ndiyo imani ya uhakika, lakini pia siamini kwamba kuna uwezekano wa kumlazimisha mtu kubadili dini" alisema Wasteney.

"Lakini namna suala lilivyochukuliwa na uongozi nimeonekana kama mjinga wa dini, nataka ifahamike kwamba kuna tabia isiyoridhisha juu ya wakristo katika baadhi ya maeneo ya kazi katika sekta ya serikali" alimalizia Wasteney. Ambapo kwa upande wake NHS hawakutaka kuzungumzia lolote juu ya madai hayo kwakuwa muhusika alikuwa amefungua kesi mahakamani.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.