CHAGUO LA GK VIDEO MPYA KUTOKA KWA MWIMBAJI CHAGUO LA WATANZANIA 2014

Ambwene Mwasongwe
Ni jumapili ya tatu tangu tuanze mwaka 2015. Karibu katika chaguo la GK leo tupo kwa mwimbaji ambaye GK inathubutu kusema ndiye chaguo la Watanzania kwa mwaka 2013 na 2014 kutokana na album yake kuwabariki wengi hasa ujumbe uliomo kwenye nyimbo zake.

Huyu si mwingine bali ni mwanakaka Ambwene Mwasongwe ambaye kwasasa ni mwanafunzi wa chuo cha Uhasibu mkoani Mbeya. Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zilizofanywa na watangazaji pamoja na watu binafsi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mwimbaji wa injili anayewabariki na kuwagusa kupitia nyimbo zake asilimia 80 wamemtaja Ambwene.

Leo tumekuchagulia wimbo 'Mzee Wa Siku' unaopatikana katika album yake iliyopita, ingawa video ni mpya kutokana na mwimbaji huyo kurekodi video ya album hiyo hivi karibuni. Tunakutakia jumapili njema yenye baraka. Ubarikiwe


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.